|
Mkurugenzi
Mtendaji wa Ikolo Investment Ltd Bw. Maggid Mjengwa akizungumza na waandishi wa
habari (hawapo pichani) kuhusu mdahalo wa Diaspora kuhusu uchumi na maendeleo
ya Taifa leo Jijini Dar es Salaam. Mdahalo huo utafanyika tarehe 11 mwezi April
katika Ukumbi wa Mzalendo Pub uliopo Kijitonyama Jijini Dar es Salaam. Kushoto
ni Mratibu wa Vikoba Kimataifa Bw. Mwinyirwaka Hatibu. |
|
Mratibu
wa Vikoba Kimataifa Bw. Mwinyirwaka Hatibu akifafanua jambo na waandishi wa habari
(hawapo pichani) kuhusu mdahalo wa Diaspora kuhusu uchumi na maendeleo ya Taifa
leo Jijini Dar es Salaam. Mdahalo huo utafanyika tarehe 11 mwezi April katika
Ukumbi wa Mzalendo Pub uliopo Kijitonyama Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Ikolo Investment Ltd Bw. Maggid Mjengwa.
|
|
Baadhi
ya waandishi wa habari wakifatilia uongozi wa Ikolo Investiment LTD wakati wa
mkutano wao na waandishi wa habari kuhusu mdahalo wa Diaspora leo jijini Dar es
Salaam.
Picha na: Frank Shija
|
Habari na: Nuru Juma &
Husna Saidi
WATANZANIA waalikwa kushiriki
katika mdahalo baina ya Diaspora na wenzao waishio nchini ili kujadili nafasi ya
Diaspora katika uchumi wa nchi, unaotarajiwa kufanyika tarehe 11 na 12 April
katika ukumbi wa Mzalendo Pub Jijini Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa na
Mkurugenzi wa kampuni ya Ikolo
Investiment Bw Maggid Mjengwa wakati akiongea na waandishi wa habari, leo
jijini Dar es Salaam.
Mjengwa amesema kuwa
Mdahalo huo umeandaliwa kwa lengo mahususi la kuwakutanisha kwa pamoja wadau wa
maendeleo kwa ajili ya kusukuma mbele jitihada za kuifanya Tanzania kuwa nchi
ya uchumi wa viwanda.
“Lengo la mdahalo huu
ni kuwakutanisha watanzania waliopo Ughaibuni, watanzania waliokua wakiishi
Ughaibuni na kwa sasa wamerudi na watanzania ambao hawakuwahi kufika Ughaibuni
ili kuweza kujadili maendeleo ya nchi” alisema Mjengwa.
Aliongeza kuwa katika
mdahalo huo pia utatumika kama sehemu ya maadhimisho ya miaka kumi ya
kuanzishwa kwa mtandao wa Mjengwa Blog, mtandao ambao kimsingi ndiyo umekuwa
daraja la kuwakutanisha Diaspora.
“Mdahalo huu ni
pamoja na kuadhimisha miaka kumi ya Mjengwa Blog hivyo tumeona kuyafanya
maadhimisho hayo kuwa ya tofauti kwa utofauti
kuwajumuisha watanzania kujadili kwa pamoja mambo kadhaa kuhusu uchumi
kwa lengo la kufanikisha maendeleo ya nchi kwa haraka zaidi.” Alisisitiza.
Nae Mratibu wa Vikoba
Kimataifa Mwinyirwaka Hatibu alisema
mdahalo huo pia utahusisha na
mafunzo ya ujasiriamali kwa watanzania ili kuweza kufanikiwa kimaisha binafsi
na kufanikiwa kwa taifa kiujumla.
“Katika kuhakikisha
Tanzania inanufaika na Diaspora,yapata miaka mitatu sasa Serikali imekuwa ikiendesha
mikutano kama hii kila mwezi wa nane kwa kuwaita watanzania waishio nje ya nchi
kujadili uchumi na maendeleo ya nchi na kwa mara ya mwisho mkutano kama huu
ulifanyika Zanzibar” alisema Hatibu.
Hata hivyo aliwasihi
wanahabari na wananchi kwa ujumla kufika katika tukio hilo kwani watapata fursa
ya kukutana na watu kutoka mataifa mbalimbali na kuweza kujifunza vitu vingi
kutoka kwao.