Serikali
kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana imetoa mikopo yenye thamani ya Shillingi
Billioni 1.5 kwa vikundi vya vijana 129 katika Halmashauri mbalimbali nchini.
Hayo
yamebainishwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa
alipokuwa akitoa hotuba kuhusu mapitio na mwelekeo wa kazi za Serikali na
makadirio ya mapato na matumizi ya fedha
za Ofisi yake kwa mwaka wa Fedha 2017/2018.
“Serikali
inaendelea na azma yake ya kuwawezesha vijana kujikwamua kiuchumi kwa kutoa
mikopo yenye riba nafuu”’ Alisisitiza Mhe. Majaliwa.
Aidha
, Mamlaka za Serikali za Mitaa kupitia mapato yake ya ndani zimetoa Shillingi
Billioni 4.6 ikiwa ni mikopo yenye masharti nafuu kwa vikundi vya vijana 2,356
na hatua hizi zimekwenda sanjari na utengeji wa maeneo maalum yenye jumla ya
ekari 85,603 kwa ajili ya shughuli za vijana za Kilimo, biashara ndogo ndogo,
burudani na michezo.
Katika
mwaka 2017/2018, Serikali itaendelea kusimamia Halmashauri zote nchini kutenga
asilmia 5 ya mapato yao kwa ajili ya vijana na asilimia 5 kwa wanawake.