TAASISI YA AGA KHAN YAFUNGUA KITUO CHA AFYA KATA YA MBAGALA JIJINI DAR.

Na James Salvatory  Dar
Katika kuendeleza juhudi za kuunga mkono serikali  ya awamu ya tano  katika sekta ya afya, taasisi ya huduma za afya ya Aga Khan imefungua kituo cha afya katika kata ya Mbagala ili kuwasaidia wakazi  wa kata hiyo na maeneo jirani katika kupata huduma za afya.

Akizungumza jana Mbagala Zachiem  Jijini Dar es salaam katika uzinduzi wa  kituo hicho  cha afya, Mkurungezi wa hospitali ya Aga Khani Otion Road, Dkt.Mustaaf Bapumia alisema kuwa dhamira yao kama taasisi ya huduma za afya ni kuhakikisa wanafungua vituo  35 nchi  zima ifikapo disemba 2018  ambazo zitakuwa zikitoa huduma bora ,angalizi nafuu na za kudumu kwa wanzania wote

Aidha alisema kuwa agakhan Tanzania itakuwa ni ya kwanza katika sekta binafsi kuweka misingi madhubuti ya mfumo bora wa afya inayoanzia katika ngazi za wilaya na kuelekea kuwa hospitali kuu ya rufaa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa wauguzi kutoka hospitali hiyo Lucy Hwai alisema kuwa wauguzi wa hospitali hiyo wako vizuri kwani wanavyotoka katika vyuo hupewa mafunzo mengine ili kuendana na huduma za agakhani
Powered by Blogger.