JUKWAA LA KATIBA LAISHAURI SERIKALI KUHUSU MCHAKATO WA KATIBA MPYA.

James Salvatory-Dar
Jukwaa la Katiba Tanzania (JUKATA)  imeishauri serikali kutoa taarifa rasmi kwenye gazeti la serikali kwamba mchakato wa katiba ni hai  na utaendelea tena ili kupata  katiba mpya.

Akizungumza na wandishi wa habari Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mtendaji  wa jukwaa hilo, Hebron Mwakahenda alisema kuwa katika bunge  hili la April  2017, waziri husika apeleke miswada ya marekebisho ya sheria ili kurekebisha sheria zinazosimamia mchakato wa katiba mpya ikiwa ni pamoja na sheria ya kuanisha ni hatua gani  za kupitia kifikia katiba mpya ikiwemo kuundwa  chombo cha kusimamia mchakato wa katiba mpya 

Aidha alisema kuwa ni vema serikali kabla ya kurekebisha sheria  iwape fursa wananchi kujadili kwa kina ili kama taifa kukubaliana  masuala ya msingi ya kuingizwa kwenye marekebisho  na kuruhusu mijadala ya wazi juu yamaudhi ya katiba inayopendekezwa kwa sababu maudhui yake yamewagawa watanzania badala ya kuwaunganisha  likiwa  lengo la katiba ni kuwaunganisha watu na sio  kujenga makundi ,chuki na uhasama  pia busara kufikia muafaka wa kitaifa kwenye masuala msingi ya katiba kama vile haki za binadamu,muungano, maadili na miiko ya uongozi na usawa wa kijinsia.

Katika hatua nyingine Mwakahenda alisema kuwa wamesikitishwa na kitendo cha serikali kutotenga fedha tena kwa mwaka wa pili kwa ajili ya kukamilisha mchakato wa katiba na kuishauri serikali itenge fedha katika bajeti ya wizara mwaka wa fedha 2017/2018  ili kukamilisha mchakato wa katiba mpya kwa vile muda muafaka wa kumaliza uandishi wa katiba mpya ni kati ya mwaka 2017 na 2018  tofauti na hapo Upo uwezekano mkubwa katiba mpya ikapatikana baada ya mwaka 2020 hii ni kwa sababu 2019 na 2020 ni miaka ya yenye uchaguzi na uzoefu inaonyesha siyo rahisi kuandika katiba karibu na kipindi cha uchaguzi  ama wakati wa uchaguzi.
Powered by Blogger.