SIMBA WAJIANDAE, BOCCO SASA YUKO VIZURI NA TAYARI KWA KAZI YA JUMAMOSI


Kati ya mechi zinazosubiriwa kwa hamu ni Simba dhidi ya Azam FC na itakuwa mechi ya Kombe la Shirikisho.

Mechi hiyo itapigwa Jumamosi na wanachojivunia Azam FC kwa sasa ni kurejea kwa nahodha wao, John Bocco.


Bocco amerejea mazoezi siku chache zilizopita baada ya kuungana na wenzake.


Kabla alianza mazoezi ya taratibu akifanya peke yake chini ya uangalizi wa daktari.

Lakini sasa Bocco yuko fiti ameungana na wenzake ambao amekuwa akifanya nao mazoezi pamoja.


Bocco ni tishio kwa Simba na Yanga kutokana na uwezo wake mkubwa wa kupachika mabao kila anapokutana na timu hizo.
Powered by Blogger.