COSTA "MUNYAMA" ALIVYOFIKISHA MABAO 50 YA LIGI KUU ENGLAND
Mshambuliaji Diego Costa wa Chelsea, jana alifunga bao la 50 akiwa na kikosi hicho chino ya Kocha, Antonio Conte.
Costa
alifunga mabao mawili wakati Chelsea ikiitwanga Southampton kwa mabao
4-2 katika mechi ya Ligi Kuu England kwenye Uwanja wa Stamford Bridge,
London.
Wakati
anafunga mabao hayo mawili, Costa alikuwa anaandamwa na ukame wa
kupachika mabao baada ya kucheza mechi tano bila kufunga hata bao moja.
Costa
hakuwa amewahi kucheza mechi tano bila kufunga tokea msimu wa 2012-13
alipocheza mechi sita bila kufunga hata bao moja katika La Liga akiwa na
Atletico Madrid.
Imemchukua mechi 85 kufikisha mabao 50 ya Ligi Kuu England.
Wengine
ambao waliowahi kufunga mabao 50 ya Ligi Kuu England na mechi
walizocheza kwenye mabao huku Any Cole akiwa ndiye aliyefunga mabao 50
katika mechi chache au haraka zaidi.
Andy Cole (65)
Alan Shearer (66)
Ruud van Nistelrooy (68)
Fernando Torres (72)
Sergio Aguero (81)
Thierry Henry (83)
Kevin Phillips (83)