RAIS MAGUFULI AWANYEMELEA WATUMISHI SERIKALINI WENYE VYETI FEKI
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania,John Pombe Joseph Magufuli,amejinasibu kutenda haki mara
atapopata ripoti ya watumishi wa Serikali,waliogushi vyeti.
Kuna madai ya wafanyakazi wa Serikali zaidi ya elfu tisa kutumia vyeti
vya kufoji,ambapo sasa Rais Magufuli, amefunguka kwa kusema sasa
anasubiri ripoti ya wahusika hao ili aitendee kazi.
Rais Magufuli amesema hayo, wakati akizindua majengo ya Hostel za Chuo
Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM),kwa kudai kumekuwa na changamoto kubwa
katika kila sekta hivyo sasa anasubiri hiyo ripoti ili aweze kuifanyika
kazi na kutenda haki katika jambo hilo.
Anasema;"Naisubiri ripoti ya wafanyakazi wa Serikali zaidi ya elfu tisa ambao wana vyeti vya kufoji ili niifanyie kazi."
Mbali na hilo Rais Magufuli ameitaka Taasisi ya TCU kuacha kuwapangia
wanafunzi vyuo bali wanafunzi wanapaswa kuwa huru kuchagua aina ya vyuo
ambavyo wao wanataka kwenda kusoma.
Amefafanua kwa kusema kufanya hivyo itatoa nafasi kila chuo kuwa na
wanafunzi wa kutosha huku wanafunzi pia wakienda kusoma sehemu ambazo
wao wanahitaji kwenda kusoma na si kuwapangia.
"Mtu amefaulu ana sifa zake anataka kuja kusoma Chuo Kikuu Cha Dar es
Salaam afaidi mabweni ya Magufuli analazimishwa kupelekwa kwenye ka chuo
ambako wala hakana jina hata ukitafuta kwenye mtandao hakaonekani,
akasome pale wakati hawana hata mabweni na saa zingine hata walimu
hawana, tunawatesa watoto hawa,”
“… na saa zingine wakuu wa vyuo vile wamekuwa na tabia ya kwenda kwenye
uongozi wa TCU ingawa sina ushahidi wapangiwe idadi wa wanafunzi
wanaowataka kwenye vyuo hivyo,”
“….sifahamu wanapangiwa kwa rushwa,lakini wapo pia kuna ushahidi na
baadhi ya viongozi wa vyuo fulani fulani waliofunga safari kwenda TCU
kwa ajili ya kuomba wapangiwe wanafunzi au kutoa shukrani, au hata
kwenda kuwasalimu tu" alisema Rais Magufuli.