PROF. ELISANTE OLE GABRIEL AWAOMBA WADHAMINI KUJITOKEZA KUDHAMINI MICHEZO YA WANAWAKE



Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza na Wanawake  (hawapo pichani ) leo Jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Kongamano la Wanawake na Michezo lilioandaliwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT).Kushoto ni Mjumbe wa Baraza hilo Bibi Jenifer Mmasi.

Mjumbe wa Baraza la Michezo la Taifa  Bibi Jenifer Mmasi akitoa maelezo kuhusu Kongamano  la Wanawake na Michezo liliondaliwa na Baraza hilo leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni  Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanawake walioshiriki  Kongamano la Wanawake na Michezo lilioandaliwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) mara baada ya kuzindua kongamano hilo leo Jijini Dar es Salaam.


Picha na Shamimu Nyaki


Na Shamimu Nyaki


Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel ameomba wadhamini kujitokeza kudhamini michezo ya wanawake ili itambulike na kupata  mafanikio  hapa nchini.


Kauli hiyo ameitoa leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa anazindua Kongamano la wanawake na Michezo liliondaliwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ambapo  amesema kuwa michezo inahitaji msaada mkubwa kutoka kwa wadhamini  hivyo ni wajibu kwa wadhamini mbalimbali kuona jitihada zinazooneshwa na wanawake na  waziunge mkono.


“Michezo inaleta ni afya lakini pia in

aleta umoja na ushirikiano katika kutafuta maendeleo ya jamii nawaomba wadhamini mjitokeze kuunga mkono jitihada hizi za wanawake ili  zilete  mafanikio,” Alesema Prof  Elisante  Ole Gabriel.


Aidha Katibu Mkuu huyo amewataka viongoz

i wa vyama vya michezo vya wanawake kuwa wabunifu katika kutafuta fursa zilizopo katika michezo ili waweze kufanikiwa zaidi pamoja na kusimamia yale waliyoazimia kwa maendeleo ya Michezo yao.


Kwa upande wake Bibi Jenifer Mmasi Mjumbe wa Baraza la Michezo la Taifa amesema kuwa kongamano hilo lina lengo la kuwakutanisha wanawake ambao ni wanamichezo kupata ujuzi na namna bora ya kutumia michezo katika jamii zao kama njia ya kutatua changamoto malimbali za maendeleo.

“Ni vizuri kwenu viongozi kutumia 

fursa hii kujifunza zaidi ili mnapokuwa katika maeneo yenu muwaelimishe wanawake wengine umuhimu wa kushiriki katika michezo,”Alisema  Bibi Jenifer.


Kongamano hilo la siku moja linalenga kujadili jinsi wanawake wanavyoweza kufanikiwa kupitia michezo pamoja na changamoto ambazo wanawake wanakutana nazo katika kushiriki michezo  na kuzitafutia  ufumbuzi.


Powered by Blogger.