KAULI YA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI MWIGULU NCHEMBA KUPOTEA KWA ROMA MKATOLIKI
Usiku wa April 5 2017 taarifa za kukamatwa kwa msanii wa hip hop Roma
Mkatolikia zilianza kuenea katika mitandao ya kijamii kwa kuandikwa kuwa
Roma Mkatoliki na Moni wakiwa studio za Tongwe Records walikuja
kukamatwa na watu wasiojulikana na kuwapeleka kusikojulikana.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba ambaye ndio anahusika
na usalama wa raia, ametumia ukurasa wake wa instagram kuonesha kuguswa
na tukio la kutekwa kwa Roma Mkatoliki na Moni, Waziri Nchemba ameeleza
kuwa amewaagiza polisi kufuatilia na kutoa taarifa kwa umma.
“Nimeshtushwa kwa kutokuonekana kwa Msanii Roma na Wenzake mpaka sasa.
Nimeshtuka zaidi nilipofuatilia na kuambiwa hakuna kituo chochote cha
polisi kinachowashikilia. Nimeelekeza Polisi wafuatilie kwa karibu kujua
undani wa tukio hili na hatima yao na kutoa taarifa kwa umma”