PICHA KATIKA MATUKIO :CCM MKOA WA MARA HATUTAFUMBIA MACHO VIONGOZI WATAKAO TUMIA FEDHA KATIKA UCHAGUZI.

Katibu wa chama cha Mapinduzi  (CCM)Mkoani Mara  Innocent Nanzabar akisisitiza jambo katika kikao cha Halmashauri kuu ya chama Wilayani Rorya  Mkoani Mara.


Katibu wa chama cha Mapinduzi Wilayani Rorya Mkoani Mara Lucy Bonephace akisisitiza jambo kuhusua ziara ambayo ilifanyika katika kata zote wilayani humo kwa lengo la kutoa maelekezo kwa viongozi kuhusu uchaguzi pamoja na suala zima la kuunganisha Matawi.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilayani Rorya Mkoani Mara Samwel kiboye NO3 kulia akiteta jambo na katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mara Innocent Nanzabar katika kikao cha Halmashauri kuu ya chama


Wajumbe wa Halmashauri kuu wakiwa katika kikao Wilayani Rorya Mkoani Mara.


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilayani Rorya Mkoani Mara Samwel Kiboye N03 akisistiza jambo katika kikao cha  Halmashauri kuu Mwenyekiti huyo amemwakikishia katibu wa Mkoa CCM kuwa viongozi watakao teuliwa kwa ajili ya uchaguzi wa Matawi ni wale wenye sifa zote za uongozi na wanaopenda kutumikia vyema Chama hicho na kulaani vikali viongzi ambao wamepuuzia maagizo ya chama makao makuu.

Katibu Wazazi Mkoa wa Mara Robert Manjebe akisistiza jambo katika kikao hicho ambapo amewataka wanachama wa Chama hicho kuendelea kufuata katiba ya chama hicho ikiwa ni pamoja na kutekeleza ilani ya chama Hicho.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF Wilayani Rorya Mkoani Mara George Agano  baada ya kujiunga na Chama cha Mapinduzi Wilayani Rorya Mkoani Mara.



Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF Wilayani Rorya Mkoani Mara George Agano baada ya kujiunga CCM akisalimiana na Katibu wa CCM Mkoa wa Mara Innocent Nanzabar.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF Wilayani Rorya Mkoani Mara George Agano akisalima na Mwenyekiti wa CCM Wilayani Rorya Mkoani Mara Samwel Kiboye.


Katibu wa CCM Mkoa wa Mara Innocent Nanzabar amesema kuwa Chama hakitavumilia Viongozi ambao watatumia pesa katika chaguzi zozote ili kuendelea kulinda heshima ya Chama hicho.

 


"Lengo letu ni kuhakikisha kila mtu mwenye sifa ya kuwa kiongozi anapasa nafasi hiyo lakini kiongozi wa fedha chama hakitakubaliana naye bora habaki na fedha zake lakini chama kibaki" salama alisema Innocent.

Aidha kiongozi wa chama hicho aliongeza kuwa viongozi wote watakaobainika kutumia rushwa majina yao hayatarudi kutoka mkoani kwa sababu wamekiuka maadili na taratibu za chama hicho.

PICHA ZOTE NA CLEO24NEWS UKIWA NA HABARI, MATANGAZO PIGA SIMU NO 0766424928

Powered by Blogger.