UNA HOFU NA JOHN BOCCO, SIMBA WATOA KAULI YAO WAKISISITIZA "AJE"
Azam
FC ina furaha baada ya kurejea uwanjani kwa straika wake John Bocco,
lakini Simba imesema hata kama mchezaji huyo atacheza leo dhidi yao, ni
lazima wao washinde.
Bocco
alikuwa nje ya uwanja kwa muda akiuguza majeraha ya nyama za paja na
ndiye aliyeifungia Azam dhidi ya Simba katika ushindi wa bao 1-0 wa timu
yake katika Ligi Kuu Bara Januari 28, mwaka huu. Simba pia ilifungwa
bao 1-0 katika fainali ya Kombe la Mapinduzi mwaka huu.
Leo
Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Simba inacheza na Azam
mechi ya nusu fainali ya Kombe la FA ambapo mshindi atacheza fainali ya
michuano hiyo.
Kocha
Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja, amesema wanathamini mchango wa
Bocco kwa timu yake lakini watapambana ili washinde mchezo huo.
“Najua
Azam wanategemea nafasi hii pekee ili wacheze Kombe la Shirikisho
Afrika mwakani, hawa tunawafunga na hawatacheza mechi za kimataifa
mwakani, hii ni nafasi yetu.
“Hawatapanda
ndege msimu ujao kwani tunataka kuwabania nafasi hii ya FA wanayoitaka
na tunataka kulipa kisasi kwani Azam wametufunga mara mbili mwaka huu,”
alisema Mayanja.