MAMBO YA NYOSSO YAIBUKA URUGUAY, MSHAMBULIZI WA CHAPECOENSE YA BRAZIL AMPAPASA MWENZAKE MAKALIO
Mshambuliaji
nyota wa Chapecoense ya Brazil, Rossi amelambwa kadi nyekundu na
kutolewa nje katika mechi ya Kombe la Liberatadores dhidi ya Club Nacional ya Uruguay.
Katika mechi hiyo, Nacional walikuwa nyumbani jijini Montevideo, Uruguay.
Rossi
alitolewa nje kwa kulambwa kadi nyekundu baada ya kumshika makalio beki
wa Club Nacional kama ambavyo beki Juma Nyosso akiwa Mbeya City
alivyowahi kumfanyia Elius Maguri wa Simba wakati huo.
Chapecoense ni ile timu ya Brazil ambayo wachezaji wake walipoteza maisha kwenye ajali ya ndege hivi karibuni.
Kikosi
cha Chapecoense, tayari kilikuwa kimelala kwa mabao 3-0 na Rossi aliona
hakukuwa na ujanja zaidi ya kutumia njia za ziada.