MOTO WAZUKA SOKO LA WAFANYABIASHARA NA WAKULIMA REBU WILAYANI TARIME.

Usiku wa kuamkia leo jumamosi, April 15,2017, kumezuka moto katika mabanda na maduka yaliyo katika Soko la wafanyabiashara na Wakulima wa nafaka, matunda, mazao na bidhaa mbalimbali ikiwemo nguo na viatu, la Rebu wilaya ya Tarime mkoani Mara.


Licha ya moto huo kuzimwa, bado zoezi hilo lilikumbwa na changamoto kadhaa ikiwemo ukosefu wa maji na baadhi ya wananchi kutokomea na mali huku BMG ikishindwa kufahamu ikiwa jeshi la zima moto limepata taarifa ya tukio hilo ili kufika kusaidia.


Bado chanzo cha moto huo hakijafahamika ikiwa ni pamoja na thamani halisi ya hasara iliyopatikana.

Picha na Makoba BMGHabari

Powered by Blogger.