Mbunge wa Buyungu Mhe. Kasuku Bilago(kushoto)
Mbunge wa Kiwani (Zanzibar) Mhe. Abdalla Haji Ali(katikati) pamoja na Mbunge wa Mtera
Mhe. Livingstone Lusinde(kulia) wakijadiliana jambo na kupongezana mara baada ya kumalizika kwa mazoezi katika
viwanja vya Kilimani Mjini Dodoma.
Picha/Habari na Raymond Mushumbusi
Ofisi
ya Rais TAMISEMI na baadhi ya wabunge wameongoza vikundi vya Jogging Mkoani Dodoma
kufanya mazoezi kuunga mkono agizo la Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Mama Samia Sluhu Hassan wa kufanya mazoezi.
Akizungumza
baada ya mazoezi hayo Afisa Tawala
kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Bibi Rose Lugendo amewaomba wakazi wa Dodoma
wajitokeze kwa wingi kufanya mazoezi kwa afya zao na kuimarisha mahusiano baina
yao.
“Napenda
kuwashauri wakazi wa Dodoma kujiunga na Jogging Clubs na kuwa na Utamaduni wa
kufanya mazoezi kwa Afya zao” alisisitiza Bibi Rose.
Kwa
upande wake Mbunge Wa Mtera Mhe. Livingstone Lusinde amewaasa vijana kujitokeza
kufanya mazoezi kila siku na sio kusubiri kufanya mazoezi mara moja kwa mwezi
kwasababu mazoezi ni sehemu ya maisha.
“Vijana
tumieni fursa hii kufanya mazoezi na kujenga afya zenu mazoezi yawe sehemu ya
maisha yenu” alisisitiza Mhe. Lusinde.
Naye
Mbunge wa Buyungu Mhe. Kasuku Bilago amevipongeza vikundi vya Jogging Dodoma
kwa kuleta mwamko wa mazoezi katika mkoa wao na kujenga desturi ya watu kupenda
mazoezi na michezo.
Aidha
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Dodoma Mjini Daniel Shija amewahakikishia ulinzi wanamazoezi
na michezo kwa ujumla katika sehemu mbalimblai ambazo watakuwa wanafanya
michezo.
|