MBAO FC, PRISONS KUWEKA REKODI KUWA ZA KWANZA KUCHEZA NYAMAGANA YENYE NYASI BANDIA
MBAO FC |
Mechi
ya Ligi Kuu Bara kati ya Mbao FC dhidi ya Tanzania Prison kesho, sasa
itachezwa kwenye uwanja usio na majukwaa wa Nyamgana ambao uko katikati
ya jiji la Mwanza.
Imeelezwa katika uwanja wa CCM Kirumba kuna matamasha ambayo yamelazimu mchezo huo kuhamishwa.
Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Mwanza (MZFA), Leonard Malongo amesema imelazimika kuwa hivyo.
“Hatuna ujanja, sasa hii mechi ya kesho Jumapili itachezwa Nyamagana,” alisema.
Kama
ni hivyo, maana yake Mbao FC na Prisons zinaandika rekodi ya kuwa timu
za kwanza kucheza katika uwanja huo tokea uwekewe nyasi bandia.