KAMPENI YA "KOMBOA POINTI ZA KAGERA" YAZINDULIWA, KATIBU MKUU TFF AMBAYE NI MWANACHAMA WA YANGA AITISHA KIKAO CHA KAMATI JUMANNE
Aliyewahi
kuwa Katibu Mkuu wa Yanga, Mwesigwa Celestine ambaye sasa ni katibu
mkuu wa TFF, ameitisha kikao cha kamati ya Kamati ya Sheria, Katiba na
Hadhi za Waehezaji ambacho kinaelezwa kimepewa jina la “komboa pointi za
Kagera”.
Taarifa
za ndani kutoka TFF zinaeleza, kikao hicho kimepangwa kufanyika Jumanne
na kuhakikisha kinarejesha “haki” ya Kagera baada ya Kamati ya Saa 72
kuipa Simba pointi tatu na mabao matatu baada ya Kagera Sugar, kubainika
ilimchezesha beki Mohammed Fakhi akiwa na pointi tatu.
“Kweli
hicho kikao kimeitishwa na wajumbe wameishatumiwa email, kazi itakuwa
ni moja tu kuipa Kagera pointi. Hapa nafikiri wewe hujajua ndugu yangu,
Yanga wameungana na kuhakikisha iwe isiwe pointi za Kagera zinarudi.
“Baba mwenye nyumba anataka pointi za timu yake zirudi, si unajua ndiye
mwenyekiti wa soka Kagera.
“Wakati
haya yanatokea, baba mwenye nyumba hakuwepo, alikuwa Morocco. Sasa
amerudi na anataka pointi zirudi. Hapa kuna Uyanga, kumbuka viongozi
wote wa juu ni Yanga. Lakini usisahau wote wanatokea hukohuko, sasa hizi
pointi hata kama Fakhi alikuwa ana kadi tatu, zitarudi,” kilieleza
chanzo.
EMAIL YA MWESIGWA KWENDA KWA WAJUMBE:
Kikao cha Kamati ya Sheria,Katiba na Hadhi za Wachezaji
jm selestine <mjselestine@yahoo.co.uk>
To TPLB TPLB <tplb.tplb@yahoo.com>, Boniface Wambura <wambura70@gmail.com>
Cc Jamal Malinzi <jamalmalinzi@gmail.com>, Richard Sinamtwa <richardsinamtwa@gmail.com>
Friday, April 14, 2017 2:06 PM
Click to View Full HTML
Mtendaji Mkuu,
Bodi ya Ligi Kuu (TPLB).
Hii ni kukufahamisha kuwa kikao cha
dharula cha Kamati ya Sheria,Katiba na Hadhi za Wachezaji ya TFF
inategemewa kukaa siku ya Jumanne tarehe 18/04/2017 katika hoteli ya
Protea Sea View saa 4 asubuhi.Unatakiwa kufika kwenye kikao na wafuatao:
1.Joel Balisidya
2.Rose Msamila
3.Michael Ngogo
3.Match officials wote wa mchezo wa ligi
Kuu kati ya Kagera Sugar na African Lyon ie Match comm,centre ref,two
assistants na mwamuzi wa nne.
4.Viongozi wa Kagera Sugar
Kila mmoja afike na nyaraka alizo nazo
kuhusiana na mchezo huo.TFF itarudisha gharama za safari kwa wale
wanaotokea nje ya Dar Es Salaam.
Wasalaam,
Mwesigwa Joas Selestine
General Secretary
Tanzania Football Federation