MASHABIKI SIMBA WAFURIKA KATIKA MITAA YA JIJI LA MWANZA KUSAKA TIKETIKE
Mashabiki wa Simba
wamejitokeza kwa wingi katika mitaa ya jiji la Mwanza ili kupata tiketi
kwa ajili ya kwenda Uwanja wa CCM Kirumba.
Simba inawavaa
wenyeji wao Toto African kwenye uwanja huo eneo la Kirumba na wenyeji
wanajivunia rekodi ya kutofungwa na Simba, miaka saba iliyopita.
Mashabiki hao wanaonyesha kuhamasishwa na Simba kuishinda Mbao FC kwa mabao 3-2 katika mechi iliyopita.