MAVUGO SASA ATAKA KURUDISHA UTAMU WA MABAO KUPITIA TOTO AFRICAN
MAVUGO |
Ukiangalia
katika mechi tatu za nyuma za Simba za Ligi Kuu Bara, straika Laudit
Mavugo hajafunga bao lolote hivyo ametamba kupambana ili afunge bao leo
dhidi ya Toto African kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa.
Akizungumza
baada ya mazoezi ya jana Ijumaa asubuhi uwanjani hapo, Mavugo raia wa
Burundi alisema sasa ni wakati wa kujituma kuliko wakati wowote ndani ya
Simba.
“Sasa
tuna presha kubwa sana ya ubingwa, huu ni wakati wetu sisi wachezaji
hasa washambuliaji kuhakikisha kuwa tunafunga mabao na kuipa ushindi
timu yetu ili itwae ubingwa.
“Sijafunga
katika mechi kadhaa huko nyuma, hivyo nitapambana ili nipate bao katika
mchezo huu kama nitapata nafasi ya kucheza,” alisema Mavugo mwenye
mabao saba katika ligi kuu.
“Nimesikia
kwa miaka nenda rudi Toto imekuwa ikiifunga sana Simba lakini niseme
kwamba mimi kwa kushirikiana na wachezaji wenzangu tumepania sana
kuifunga Toto,” alisema Mavugo raia wa Burundi.
Kabla
ya hapo, Mavugo aliyejiunga na Simba akitokea Vital'O ya Burundi ndiye
alikuwa chachu katika ufungaji katika kikosi cha Simba.