MZEE AKILIMALI ACHARUKA POINTI TATU ZA KAGERA, ASEMA HIYO NI HARAMU KABISA!
Kamati
ya Saa 72 ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) iliipa Simba pointi tatu
baada ya kubainika Kagera Sugar ilimchezesha Mohammed Fakhi mwenye kadi
tatu za njano katika mchezo wao ulioisha kwa Simba kufungwa mabao 2-1.
Sasa
Katibu wa Baraza la Wazee wa Yanga, Mzee Ibrahim Akilimali ameibuka na
kusema, TFF imefanya kitendo cha ajabu cha kukubali kuwapa Simba pointi
za haramu na wao hawataweza kukubali. Kutokana na pointi ilizopewa,
Simba sasa ipo kileleni katika msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi
61 ikifuatiwa na Yanga yenye pointi 56. Hata hivyo, Yanga ina mchezo
mmoja mkononi.
Mzee
Akilimali alisema, wao hawatetei kwa kuwa wana ushindani wa kuwania
ubingwa na Simba, isipokuwa wanachotaka haki itendeke kwa wote na siyo
kwa baadhi tu.
“Kiukweli
nikiwa kama Katibu wa Wazee wa Yanga hatukubaliani na kitendo cha TFF
kuwapa hizo pointi za haramu Simba, siyo kwamba wote tunawania ubingwa,
hapana, isipokuwa tunataka haki itendeke.
“Haiwezekani
timu nzima washindwe kuwa na taarifa sahihi hivyo lazima tutaenda
mbele, binafsi mimi ni msemaji wa wazee wenzangu ambao nipo pamoja na
viongozi wangu wa juu wa kutaka kuona uchunguzi wa kina ili ukweli
ujulikane.
"Lakini
tutaandamana hadi kwa waziri halafu mahakamani wao si wamemwaga mboga,
sisi tunamwaga ugali ili nchi ifungiwe kabisa na Fifa (Shirikisho la
Soka la Kimataifa),” alisema Mzee Akilimali.