MANARA AJIANDAA KUKATA RUFAA KUPINGA ADHABU ALIYOPEWA NA TFF
Msemaji wa Simba, Haji Manara, atakata rufaa kupinga adhabu ya kufungiwa mwaka mmoja.
Kama ya Nidhamu ya TFF, imemfungia
Manara mwaka mzima na kumpiga faini ya Sh milioni 9, hali iliyowashitua
wadau wengi wa soka nchini.
Lakini rafiki wa karibu wa Manara ameioambia SALEHJEMBE kuwa Manara atakata rufaa.
"Namjua Haji, ni mbishi na hawezi kukubali. Laizma atakata furaa katika hili.
"Pia nimemsikia akisema hatakubali kuonewa, hali inayonifanya niamini lazima atakata rufaa," kilieleza chanzo.
Kamati hiyo imemfungia Manara kwa madai
ya utovu wa nidhamu, jambo ambalo yeye amelipinga kabisa akilinganisha
ya uonevu wa wazi.