MASHABIKI, WANACHAMA YANGA WAANZA KUCHANGA, UONGOZI WAELEZA UTAKAVYOFANYA
Mashabiki wa Yanga wameanza kuonyesha mwamko kuichangia klabu yao baada ya ombi la uongozi kuwaomba wafanye hivyo.
Hata hivyo, uongozi huo umesema kila baada ya wiki utakuwa utakuwa ukitoa taarifa kuelezea kinachoendelea.
Ifuatayo ni taarifa iliyotolewa na uongozi wa Yanga, leo.
TAARIFA KWA UMMA:
Klabu
ya soka ya Yanga SC kupitia Katibu Mkuu Charles Boniphace Mkwasa
inashukuru sana kwani zoezi la uchangiaji toka kwa wanachama limekuwa
zuri na likiendelea vyema.
Pia
uongozi utakuwa ukitoa taarifa ya makusanyo kwa wanachama wake kila
baada ya wiki moja ili waweze kufahamu mwenendo wa michango yao kwa
klabu.
Klabu
ina thamini mtu wa kipato chochote kuichangia klabu na kwa chochote
unachotoa klabu inatanguliza shukrani za dhati na kutambua umuhimu wako
katika mchakato huu.
Imetolewa na idara ya habari na mawasiliano;
Young Africans SC
25/04/2017