LUNYAMILA NAYE APIGILIA MSUMARI SUALA LA TFF KUYUMBA....
Nyota
wa zamani wa Yanga na Simba, Edibily Lunyamila amelitaka Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF) kufanya mambo kwa weledi badala ya kuangalia maslahi
binafsi kwa viongozi wake.
Lunyamila
ambaye alikuwa mchezaji tegemeo katika kikosi cha timu ya taifa,
amewataka TFF kuachana na ushabiki katika masuala ambayo yanahusiana na
haki.
“Sitaki
kuingia au kukaa upande wowote katika suala la Simba na Kagera
kuhusiana na pointi tatu. Lakini ninachosisitiza ni TFF kufanya mambo
kwa uwazi.
“Hili
suala lilikuwa lina figisu nyingi tokea mwanzo, lakini TFF
hawakuonekana ni watu waliotaka liishe kwa uwazi kwa kuanika mambo hadi
serikali ilipoingilia.
“Hii si sawa, inasababisha watu wengi zaidi kuendelea kupoteza kabisa imani na TFF,” alisema.