LWANDAMINA ANAAMINI BADO YANGA INA NAFASI YA "KUTUSUA" LAKINI.....
Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina anaamini kikosi chake kina nafasi ya kuendelea kufanya vizuri.
Lwandamina
raia wa Zambia, alifurahishwa na kiwango walichokionyesha Yanga katika
mechi ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Prisons ya Mbeya.
Lakini amesisitiza, wataendelea kufanya vizuri na kikubwa ni kuendelea kujituma.
“Mpira
ni ushindani na kila siku lakini ujitume mazoezini, ujitume katika
mechi. Ninaamini bado tuna nafasi ya kuendelea vizuri,” alisema.
Yanga ilionyesha kiwango kizuri na kuitwanga Prisons kwa mabao 3-0 katika mechi iliyokuwa ikitarajiwa kuwa ngumu kwa Yanga.