AZAM FC HAWA HAPA WAKIJIFUA TAYARI KWA MNYAMA SIMBA, JUMAMOSI
Kikosi cha Azam FC kimeendelea na mazoezi yake kama kawaida ikiwa ni pamoja na kujiandaa na Simba.
Azam FC itaivaa Simba katika mechi ya
kwanza ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho, mechi itakayopigwa kwenye
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Jumamosi.
Mazoezi ya Azam FC yamekuwa yakiendelea
kwenye Uwanja wa Azam Complex na wachezaji wakionekana wako tayari kwa
kazi dhidi ya Simba, mechi inayotarajiwa kuwa ngumu na ya kusisimua.