JUKWAA LA WAHARIRI (TEF) LAMTAKA LIPUMBA AJITOKEZE AKIRI NA KUOMBA RADHI WAANDISHI WA HABARI
Jukwaa la Wahariri nchini (TEF) limelaani kitendo cha waandishi wa
habari kujeruhiwa katika tukio la uvamizi lililotokea katika mkutano wa
CUF katika hotel ya Vina kata ya Mabibo ambapo waandishi wa habari
walipigwa na kujeruhiwa
Katika taarifa hiyo ya (TEF) imemtaka Profesa Lipumba kujitokeza na
kukiri na kuomba radhi kwa waandishi wa habari pamoja na Watanzania
kufuatia tukio hilo kama alivyofanya Maalim Seif
"Tunamtaka Profesa Lipumba binafsi atoe kauli kuhusu tukio hili kama
alivyofanya Maalim Seif ambaye binafsi aliandika barua rasmi kwa uongozi
wa TEF akilaani kupigwa kwa waandishi wa habari na kutoa pole kwa wale
waliomizwa na kupata mshtuko" Walisema viongozi wa TEF
Taarifa hiyo ya TEF ilikwenda mbali zaidi na kuwatahadharisha waandishi
wa habari, wahariri kuwa wanapaswa kuwa makini pindi wanapokuwa wanaitwa
na kundi hili la Lipumba kwa ajili ya kutoa habari zao