MANISPAA YA ILALA JIJINI DAR ES SALAAM YAOMBWA KULINUSURU DARAJA ZISISOMBWE NA MAFURIKO
Wakazi wa Gongolamboto wakipita katika daraja ambalo kingo zake
zimesombwa na mafuriko barabara ya kuelekea Machinjio ya Pugu Kajiungeni
Dar es Salaam leo.Jitihada za makusudi zisipochukuliwa daraja hilo
litasombwa na maji.
Mwonekano wa eneo hilo baada ya kusombwa na mafuriko.
Daladala likipita kwenye daraja hilo.
MANISPAA ya Ilala imeombwa kufanya jitihada za makusudi kuinusuru daraja
linaloungani eneo la Gongola mboto na Machinjio ya Pugu ambalo
lipokatika hatari ya kusombwa na maji.
Mwito huo umetolewa Dar es Salaam leo na wakazi wa Pugu Machinjioni
ambao wamesema iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa mawasiliano kati ya
wananchi wa eneo
hilo na Gongolamboto yatatoweka hivyo kuwa adha kwao kwa kufika makwao
kwa kupitia Pugu Kajiungeni badala ya barabara ya Gongo lamboto Pugu
Machinjioni kupitia kiwanda cha kutengeneza nguo cha Namera.
"Tunaomba manispaa yetu ilifanyie ukarabati daraja hili ambapo kwa
sehemu kubwa kingo zake zimesombwa na maji kutokana na mvua
zinazoendelea kunyesha " alisema Omari Mshamu mkazi wa eneo hilo.
Mkazi mwingine wa eneo hilo Marietha Stanslaus alisema iwapo daraja hilo
linasombwa na maji watakaopata shida zaidi ni wanafunzi kwani
watalazimika kutumia njia ndefu kufika mashuleni kwao kutokana kuwa
wengi wao wanasoma shule za Gongolamboto.
Jithada za kumpata diwani wa eneo hilo ili kuzungumzia suala hilo zilishindika baada ya kupiga simu yake ambayo haikupatikana.