FAHAMU KUHUSU USHIRIANO WA HALOTEL NA NMB.

 James Salvatory, Dar
Kampuni ya mawasiliano ya  Halotel na benk ya NMB  zimeingia katika ushirikiano utakaowawezesha mamilioni ya watanzania kunufaika  na huduma za kifedha nchi nzima.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Jijini Dar es salaam, Naibu  Mkurugenzi wa kampuni ya Halotel, Le  Van Dai, alisema kuwa ni hatua nyingine kubwa katika  utoaji wa huduma za kifedha kupitia simu za mkononi ambapo sasa huduma yq halopesa itakuwa imeunganishwa na benki ya NMB ili kuwawezesha wateja kufanya miamala kwa urahisi zaidi.

Kwa upande wake kaimu mkuu wa huduma Binafsi za kibenki wa NMB, Boma Raballa alisema ushirikiano huo ni mafanikio mengine makubwa ya kibiashara  kwao hususani katika kupanua  wigo wa huduma zake na namna itavyoweza kuuganisha teknolojia ili kuwarahisishia watanzania  kupata  huduma za kifedha popote walipo.
Powered by Blogger.