HEART MARATHON KUFANYIKA MUUNGANO DAY.
Katibu Mkuu wa Taasisi ya Tanzania Health Summit Bi. Rebecca John (katikati) akisisitiza jambo kwa wandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akielezea maandalizi ya mbio za heart marathon na upimaji wa afya yenye lengo la kuisaidia serikali kupunguza magonjwa yasiyoambukizika jana jijini Dar es Salaam, kushoto ni Katibu Mkuu Msaidizi wa Chama cha Riadha Tanzania Bi. Ombeni Zavara na kulia ni Katibu Mkuu Chama cha Riadha Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Lucas Nkungu. |
Katibu Mkuu Msaidizi wa Chama cha Riadha Tanzania Bi. Ombeni Zavara akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya ya mbio za heart marathon na upimaji wa afya yenye lengo la kuisaidia serikali kupunguza magonjwa yasiyoambukizika ,jana jijini Dar es Salaam, kulia ni Katibu Mkuu wa Taasisi ya Tanzania Health Summit Bi. Rebecca John. |
Mwenyekiti wa Taasisi ya Tanzania Health Summit Dkt.
Omary Chillo (kulia) akifafanua jambo
kwa wandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akielezea maandalizi ya
mbio za heart marathon na upimaji wa afya yenye lengo la kuisaidia serikali
kupunguza magonjwa yasiyoambukizika, jana jijini Dar es Salaam, katikati ni
Katibu Mkuu Chama cha Riadha Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Lucas Nkungu na kushoto
ni Katibu Mkuu wa Taasisi ya Tanzania Health Summit Bi. Rebecca John.
Na. Nuru Juma
Taasisi
ya Tanzania Health Summit yaandaa mbio za nusu Marathon na Upimaji wa afya kwa
lengo la kusaidia juhudi za serikali katika kupunguza magonjwa yasioambukiza,
mbio hizo zinazotarajia kufanyika Aprili 26 katika barabara ya Kaole iliyopo
Masaki jijini Dar es Salaam.
Hayo
yamesemwa jana na Katibu Mkuu wa Taasisi hiyo Rebecca John wakati alipokutana
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuhamasisha jamii
kushiriki.
“Kamati
ya maandalizi ya ya mbio za Heart Marathon inapenda kuwa taarifu wadau wote wa
sekta ya afya hapa nchini na jamii kwa ujumla juu ya mbio za Heart Marathon na upimaji
wa afya ili kuungana na serikali katika juhudi za kupunguza magonjwa
yasiyoambukiza” alisema Rebecca.
Aliongeza
kuwa kwa mwaka huu mbio hizi zitashirikisha washiriki zaidi ya elfu mbili
kutoka rika mbalimbali wakiwemo vijana, watoto, wazee, makundi ya watu wenye
ulemavu na watu wenye magonjwa yasiyoambukiza.
Pia
washiriki watapata nafasi ya kupima afya magonjwa mbalimbali kama vile shinikizo
la damu ,wingi wa sukari katika damu, kiasi cha mafuta mwilini, uchunguzi wa uvimbe
katika matiti na kupata ushauri wa wataalam kuhusiana na vyakula bora, magonjwa
ya moyo na mishipa ya damu.
Aidha
Bi. Rebecca aliongeza kuwa washiriki watakimbia umbali tofauti, kwani kuna mbio
ndefu za kilometa 21.1 kwa ajili ya wakimbiaji wazoefu, kilometa 10 kwa
wakimbiaji wa kati, kilometa 5 kwa wakimbiaji wa kawaida, kifamilia na kampuni
na mbio za watoto chini ya miaka 12 ni meta 700 na zawadi itatolewa kwa mshindi
wa kilometa 21.1 pekee kwa kiasi cha shilingi laki tano.
Kwa
upande wake Rais wa Tanzania Health Summit Dr.Omary Chillo alisema kuwa washiriki
watatakiwa kutoa kiasi kidogo cha fedha kwa ajili ya kununua flana pamoja na kifaaa maalum cha kuhesabia
muda wakati wa kukimbia ila maji ya kutosha yatatolewa bure kwa ajili ya
wakimbiaji.
Aliongeza
kuwa wameimarisha ulinzi kwa kushirikiana na jeshi la polisi na ili kulinda
usalama kwa washiriki na wananchi watakaokuwepo katika mashindano hayo.
“wananchi
wasiwe na wasiwasi wa usalama kwani tutashirikiana na jeshi la polisi ili
kuimarisha usalama na tumeweza kupata baraka nyingi kutoka kwao kwa kuweza
kushirikiana nao” aliongeza Chillo.
Pia Katibu msaidizi wa Chama cha Riadha nchini Bi
Ombeni Zavala alisema anashukuru wananchi wanavyoweza kujitokeza katika
mashindano hayo na pia anawaomba wananchi hasa vijana waendelee kujitokeza kwa wingi kwani wanaweza
kupata nafasi ya kuunda timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17.
Naye
Sajenti Isaya Mlokozi kutoka kanda ya usalama barabarani alisema jeshi la
polisi kikosi cha usalama barabarani litahusika vizuri katika sehem inayowahusu
kuhakikisha watu wanafanya zoezi hilo kwa hali ya usalama na litajumuika na
wananchi popote pale watakapokuwa wanakwenda.
Mashindano
haya mwaka jana yalifanyika katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam lakini kutokana
na kuongezeka kwa watu mwaka huu yatafanyikia barabara ya kaole yenye kauli
mbiu ‘piga hatua moja mbele ya magonjwa sugu’
|