Mkuu wa Mkoa wa Mara Dkt Charles Mlingwa hivi karibuni amekagua miradi mikubwa ya
kitaifa ya barabara ukiwemo ujenzi wa
barabara ya Makutano Juu- Sanzate ambayo inajengwa kwa kiwango cha rami na kusema
kukamilika kwa barabara ni muhimu kwa maendeleo ya sekta ya utalii katika Mkoa wa Mara.Mbali kurahisisha usafiri kwa wakazi wa Wilaya za
Butiama, Serengeti na Bunda , barabara hiyo itaunganisha Hifadhi ya Taifa ya
Serengeti na Ziwa Victoria na hivyo kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea Mkoa wa Mara.
|