Kutokana na kuporomoka kwa maadili
katika jamii ndoa bandia zimeibuka kwa wanawake kuolewa na wanaume wenye mali
kisha kuvunja ndoa baada ya muda mfupi na kudai kugawana mali hiyo.
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa
Nkende shuleni wilayani Tarime mkoani Mara Samwel Kisege amesema katika mtaa
wake ameamua kesi nane kwa muda wa uongozi wake na kuwa anakerwa na
kitendo cha wananwake wanaolewa na kuvunja ndoa zao kwa muda mfupi kwa lengo la
kupata mgawanyo wa mali huku yeye akisema hii ni njia mpya ya utafutaji mali
kwa wanawake.
“Sasa ninaomba nyie waandishi
mtusaidie jinsi ya kuanzisha chama cha wanaume ili kudai haki zetu kwa wanawake
hawa, maana tunadhalilika sasa, unatafuta mali mwenyewe lakini ukioa unaanza
kupata shida na wakati mwingine hata nyumba uliyojenga unashindwa kuishi ndani
yake,’alisema Kisege.
Kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu
niliokuwa mwenyekiti wa mtaa wa Nkende amekutana na kesi zaidi ya nne
imekuwa ni kama mchezo unaofanyika wa kuvunja ndoa wanawake wanaolewa na
mwanaume mwingine ikiwa lengo lao nikujitafutia mali kwa njia hiyo.
“wanaovunja ndoa ni wenye uzazi wa
watoto wawili au mmoja, kisha huolewa kwingine, imefikia wakati kwa wanawake
huwanyima hata tendo la ndoa waume zao,”alisema Kisege.
Pia inaonyesha kuwa kuwepo kwa tabia
hizi ni kutokana na wazazi kushindwa kudhibiti maadili ya watoto wao ambapo
wengi wamekuwa wakijichukulia maamzi wenyewe bila kuwashirikisha wazazi wakati
mwingine wakati wa kuolewa.
Kitendo hicho kimeonekana kuwa kibaya
kwa wanaume na jamii nzima kwani kinarudisha nyuma malengo ya mtu kwa kuwa
humfanya mwanaume kuanza maisha upya baada ya mgawanyo wa mali ambapo zamani
kwa kabila la Wakurya haikuwepo tabia hiyo.
Joseph Malele ni mmoja ya
wawanaume walionja mkasa huu alisema hamuna wanawake hao kwani
wengi wao wanahitaji mali wakati mnakubaliana kuona kutokana na maisha kuwa
magumu ndio maana wanafanya hivyo.
“Mambo yamekuwa ni magumu kwetu
wanaume kwa kuwa wanadai kuwa haki sawa, tofauti na ilivyokuwa zamani ambapo
wanaume walikuwa na sauti ya kukataa,”alisema Malele
Aidha mkazi wa mtaa wa Sabasaba
mjini Tarini Helena Peter yeye alisema kuwa ni baadhi ya wanawake ndio wamekuwa
wakitaka kugawana mali lakini wengi wao wamekuwa wakiishi vizuri na wanaume
zao.
“Siyo wote wanang’ang’ana na kuomba
mali ili wagawane mali, lakini kama nikiona mwanaume anataka kuoa mke mwingine
lazima tugawane mali, lakini siyo vizuri kutumia njia hii kujipatia mali ya
mume wako,”alisema Peter.
|