WATUMISHI WA MAHAKAMA WATAKIWA KUZINGATIA SWALA LA MUDA KATIKA UTOAJI WA HAKI ILI KUENDANA NA KAULI MBIU YA SIKU YA SHERIA DUNIANI



Wakili wa serikali Mkoani Geita,Emily Kiria akielezea namna ambavyo jamii ya wanasheria wanavyoweza kutoa haki na usawa kwa uhalisia na kwa wakati usika.

Baadhi ya mawakili wa serikali na wananchi wakiwa wanasikiliza na kufatilia kilichokuwa kikiendelea.

Wananchi wakisikiliza na kufatilia tukio lilivyokuwa likiendelea.

Wasanii wa muziki wa kizazi kipya wakitoa burudani kwenye maadhimisho hayo Mkoani Geita.

wakili kutoka chama cha mawakili Tanzania(Tanganyika law society),Bernad Otieno.akieleza namna ambavyo mahakama inatakiwa kutoa haki kwa wananchi.

Kaimu hakimu Mfawidhi wa Mkoa wa Geita,Kariho Mrisho,,akiendelea kutoa maelezo namna mahakama ilivyojipanga kuendelea kutoa haki.

Mkuu wa Mkoa wa Geita ambaye alikuwa  mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo ,Meja jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga,akisisitiza swala la maadili kwa watumishi wa mahakama Mkoani Humo. 

Lothan Simkoko akitoa neno la shukrani kwa watu ambao wamejitokeza kwenye maadhimisho hayo.

Baadhi ya mawakili wakiwa kwenye picha ya pamoja.





Jamii ya wanasheria Mkoani Geita  imetakiwa kutoa haki kwa misingi na sheria ikiwa ni pamoja na kuzingatia swala la muda kwenye kesi ambazo wanazisimamia.
Kauli hiyo imesemwa na wakili wa serikali Mkoani humo Emily Kiria  wakati wa maadhimisho ya wiki ya sheria,ambapo ameeleza kuwa jamii ya wanasheria  wote wawe wa serikali na wakujitegemea wanajukumu la kuhakikisha wanatoa haki kwa uharisia na ukweli kwa swala usika.
“Jamii ya wanasheria na hili ni jukumu la wanasheria wote wawe wa serikali au wa kujitegemea wanalo jukumu la kuhakikisha wanatoa haki kwa uharisia na kwa ukweli wa swala usika na siyo kuhakikisha tu kwamba wanawatetea au kuwasaidia watu kwasababu tu wamefika kuomba msaada”alisema Kiria

Kwa upande wake wakili kutoka chama cha mawakili Tanzania(Tanganyika law society),Bernad Otieno,alifafanua kuwa  mahakama inawajibu wa kusikiliza malalamiko yanayoletwa na wananchi na kuyatolea mahamuzi wajibu huo ni wa kikatiba kwani inatokana na jamhuri ya mwaka 1977 kama ilivyofanyiwa marekebisho katiba ibara ya 107 (A) ibara ndogo ya kwanza na ya pili.
Mkuu wa Mkoa wa Geita ambaye alikuwa  mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo ,Meja jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga ,ameendelea kusisitiza swala la muda wa kusikiliza kesi ,pamoja na  kuwataka watumishi wa mahakama  kuwa wahadilifu na waaminifu kwenye shughuli zao.
“Naomba kutoa wito kwa watumishi kuendesha kesi kwa muda usika ikiwa ni pamoja na kuwa waaminifu katika shughuli zenu za kila siku za kutoa haki kwa wananchi”alisisitiza Kyunga

Siku ya Sheria nchini ilioanzishwa mwaka 1996 ikiwa ni siku muhimu ya kuombea Majaji na Mahakimu ili kuweza kusikiliza kesi  ambapo kitaifa imefanyikia jijini Dar es salaam na Mgeni Rasmi akiwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA Dkt. John Pombe Magufuli,kauli mbiu ikiwa ni Utoaji haki kwa wakati kuwezesha ukuaji wa uchumi.

IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE
Powered by Blogger.