RAIS MAGUFULI AITAKA MAHAKAMA KUFUATILIA MADENI YA KESI SERIKALI ILIZOSHINDA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akihutubia wakati wa uzinduzi wa Mwaka Mpya wa Kimahakama katika viwanja vya Mahakama vya Mtaaa wa Chimala Ocean Road jijini Dar es salaam leo February 2, 2017 |
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA Dkt. John Pombe Magufuli ametoa wito
kwa Mahakama kukusanya Shilingi Trillioni 7.3 ambazo ni matokeo ya
serikali kushinda kesi mbalimbali za ukwepaji kodi.
Rais
Magufuli ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho
ya siku ya Sheria na Mwaka mpya wa Mahakama iliyobeba kauli Mbiu isemayo
Utoaji haki kwa wakati kuwezesha ukuaji wa uchumi.
Alisema
kuwa Takwimu zinaonesha kuwa kumekuwa na baadhi ya kesi za pingamizi za
kodi ambapo Serikali imeshinda kesi hizo japo fedha hizo
hazijakusanywa mpaka sasa.
“Kukwepa
au kutolipa kodi ni kosa kubwa sana, kila mtu anawajibu wa kulipa kodi
nchini kwa maendeleo ya nchi” nalifafanua Dkt Magufuli.
Aidha,
Rais Magufuli alisema kuwa katika kuelekea ukuaji wa uchumi, Mahakama
iwe sehemu ya chanzo cha pato la taifa kwa kwa kuhakikisha wale
wanaotakiwa kulipa fidia baada ya kushindwa kesi wanafanya hivyo pamoja
na kuwabana wakwepa kodi kwani kutimiza hilo kutaleta mabadiliko katika
uchumi wa nchi.
Katika
hatua nyingine Rais Magufuli alisema kuwa Maendeleo ya nchi hayaangalii
chama chochote, hivyo amevitaka vyombo vya utoaji haki kutoa haki kwa
usawa.
Kwa
upande wake Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma alisema
kuwa Mahakama imeandaa Mpango mkakati uliolenga kufanya maboresho ndani
ya Mahakama.
Alisema
kuwa mpango mkakati huo umelenga masuala makuu matatu ikiwemo Utawala
bora, uwajibikaji na usimamizi wa rasilimali, upatikanaji wa haki na kwa
wakati, uimarishaji wa amani kwa wananchi na ushirikishwaji wa wadau
katika shughuli za mahakama.
Aidha Kaimu Jaji Mkuu alisema kuwa Mahakama imefanikiwa kusikiliza mashauri ya kesi za uchaguzi kwa asilimia 100.
“kati
ya mashauri ya kesi 249 ikiwemo 53 za ubunge na 196 za madiwani ya
waliopinga uchaguzi kati ya kesi hizo, kesi 52 za ubunge zilikamilishwa
na kesi zote za madiwani zilikamilishwa” alifafanua Kaimu Jaji Mkuu.
Naye
Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju amesema kuwa Katiba
imeanisha bayana Kanuni ambazo zinapaswa kuzingatiwa na Mahakama wakati
ikitekeleza mamlaka yake ya utoaji haki.
“utoaji
haki mapema ipasavyo ni moja ya Kanuni ambazo Mahakama inapaswa
kuzingatia katika utekelezaji wa majukumu yake kama inavyoelekezwa
katika Katiba” alifafanua Mwanasheria Mkuu.
Alisema
kuwa Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na kufanya
biashara katika nchi ya Tanzania hivyo kuchochea maendeleo ya kiuchumi.
Siku ya Sheria nchini ilioanzishwa mwaka 1996 ikiwa ni siku muhimu ya kuombea Majaji na Mahakimu ili kuweza kusikiliza kesi.