Tazama Picha 46- MAADHIMISHO YA SIKU YA SHERIA NCHINI TANZANIA YALIVYOFANYIKA MKOA WA SHINYANGA
Alhamis Februari 2,2017-Hapa ni katika
viwanja vya Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga ambako
kumefanyika maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini Tanzania inayoashiria
uzinduzi wa mwaka mpya wa Kimahakama.
Kauli mbiu ya Siku ya Sheria nchini Tanzania Mwaka huu 2017 ni "Umuhimu wa utoaji haki kwa wakati kuwezesha ukuaji wa uchumi".
Mgeni rasmi wakati wa uzinduzi huo/maadhimisho ya siku ya sheria "Law
Day" alikuwa kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Kahama Fadhili Nkurlu
ambaye ni mkuu wa wilaya ya Kahama.
Pamoja na mambo kadha wa kadha yaliyojiri wakati wa maadhimisho
hayo,kilio kikubwa cha wadau wa mahakama kilikuwa ni umuhimu wa mahakama
kutoa haki kwa wakati kwani uchelewashaji wa utoaji haki unawafanya
wananchi washindwe kufanya shughuli za maendeleo matokeo yake kurudisha
uchumi wa nchi nyuma.
Lawama nyingi zilitupwa kwa jeshi la polisi kuwashikilia watuhumiwa kwa
muda wa zaidi ya saa 24 bila kuwafikisha mahakamani lakini pia polisi
kukwamisha kesi mahakamani kwa kuchelewa kupeleka ushahidi mahakamani.
Mahakama nayo inakanyoshewa vidole kwa baadhi ya majaji,mawakili wa
serikali,makarani na mahakimu kuendekeza rushwa,wananchi kutopewa nakala
za kesi zao kwa wakati huku wananchi nao wakilaumiwa kwa kutotoa
ushirikiano mahakamani.
Mwandishi mkuu wa Malunde1
blog,KadamaMalunde,alikuwepo eneo la tukio ametuletea picha 46 za
Matukio yaliyojiri...Tazama hapa chini
Wa kwanza kushoto ni Profesa jaji John Ruhangisa wa mahakama kuu ya
Tanzania kanda ya Shinyanga,mgeni rasmi kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga
Fadhili Nkurlu na Jaji mfawidhi wa mahakama kuu ya Tanzania kanda ya
Shinyanga Richard Kibela
Meza kuu
Kushoto ni Jaji mfawidhi wa mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Shinyanga
Richard Kibela akiteta jambo na Jaji wa Mahakama kuu ya Tanzania kanda
ya Shinyanga Victoria Makani
Wa kwanza kushoto ni Wakili wa serikali mkuu mfawidhi Shinyanga Pendo
Makondo akifuatiwa na mkuu wa wilayaya Shinyanga Josephine Matiro
akifuatiwa na Profesa jaji John Ruhangisa wa mahakama kuu ya Tanzania
kanda ya Shinyanga
Kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Fadhili Nkurlu akiteta jambo na Jaji mfawidhi wa mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Shinyanga
Sheikh mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya akiomba dua wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria nchini
Askofu wa kanisa la KKKT Emmanuel Makala akiomba dua/sala
Mahakimu na watumishi wa mahakama wakiwa eneo la tukio
Askofu wa kanisa la Anglikana akiomba dua/sala
Askofu wa kanisa la AICT Dr.John Nkola akiomba sala
Meza kuu wakiomba
Askofu wa kanisa la EAGT akiomba
Kushoto ni Mchungaji wa kanisa la SDA akiomba
Kiongozi wa dini akiomba
Kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Fadhili Nkurlu akiteta jambo na Jaji mfawidhi wa mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Shinyanga
Watumishi wa mahakama wakiwa eneo la tukio
Watumishi wa mahakama
Mahakimu wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
Mkurugenzi wa Shirika la AGAPE John Myola (aliyevaa miwani) akiwa eneo la tukio
Mgeni rasmi Fadhili Nkurlu (katikati) akitafakari jambo
Tunafuatilia kinachoendelea....
Meza kuu wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
Waaandishi wa habari wakiwa eneo la tukio
Askari polisi wakiwa eneo la tukio
Wananchi wakifuatilia kilichokuwa kinajiri
Wananchi wakiwa eneo la tukio
Tunafuatilia kinachoendelea.....
Watumishi wa mahakama na mawakili
Kaimu mwenyekiti wa Chama cha Mawakili wa Kujitegemea mkoa wa Shinyanga
Paul Kaunda akizungumza ambapo alisema nakala za hukumu hazichapwi kwa
wakati na hata zikichapwa mahakimu wamekuwa wakitumia muda mrefu
kuzifanyia uhakiki hivyo kuchelewesha azma na haki yam kata rufaa katika
mahakama za juu.
Kaunda alisema utoaji wa haki kwa wakati utasaidia kwa kiasi kikubwa
kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuja kuwekeza katika sekta
mbalimbali hapa nchini
Wakili wa serikali mkuu mfawidhi Shinyanga Pendo Makondo akizungumza
ambapo alisema endapo kesi zitaisha kwa wakati mahakamani itasaidia kwa
kiasi kikubwa kukuza uchumi wa nchi kwani wananchi watafanya shughuli
zao badala ya kuwaza kesi kila siku
Jaji mfawidhi wa mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Shinyanga Richard
Kibela akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria nchini.Jaji
Kibela alisema katika kipindi cha mwaka 2016 mahakama hiyo iliamua jumla
ya mashauri 392 yakiwa ni kati ya mashauri yaliyokuwa yamefunguliwa na
yake yaliyobaki mwaka 2015 ambayo kwa ujumla yalikuwa mashauri 1087.
Jaji Kibela alisema kesi nyingi zimerithiwa kutoka mahakama kuu ya
Tanzania kanda ya Tabora kabla ya kuanzisha kanda hii mwaka 2015
Mgeni rasmi/Kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Fadhili Nkurlu akiwahutubia
wadau wa mahakama ambapo aliisisitiza mahakama kutoa haki kwa wakati ili
wananchi waweze kufanya shughuli za maendeleo kuinua uchumi wa nchi
Kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Fadhili Nkurlu aliwaomba watanzania
kuwapuuza baadhi ya watu wanaosema kuwa mahakama zinaingiliwa kimajukumu
Kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Fadhili Nkurlu
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha watu wenye Ualbino nchini Tanzania Josephat Torner akifuatilia kilichokuwa kinaendelea
Meza kuu wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
Picha ya pamoja,mgeni rasmi,majaji ,mkuu wa wilaya ya
Shinyanga,mawakili na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa
Shinyanga na viongozi wa dini
Picha ya pamoja,mgeni rasmi,majaji,mkuu wa wilaya ya Shinyanga,mawakili na viongozi wa dini
Picha ya pamoja mgeni rasmi,majaji,mkuu wa wilaya ya Shinyanga,mawakili na mahakimu
Picha ya pamoja mgeni rasmi,majaji ,mkuu wa wilaya ya Shinyanga,mawakili na mawakili wa serikali na wa kujitegemea
Picha ya pamoja mgeni rasmi,majaji,mkuu wa wilaya ya Shinyanga,mawakili na viongozi wa taasisi mbalimbali
Picha ya pamoja mgeni rasmi,majaji,mkuu wa wilaya ya Shinyanga,mawakili na watumishi wa mahakama
Picha ya pamoja mgeni rasmi,majaji,mkuu wa wilaya ya Shinyanga,mawakili watumishi wa mahakama na wadau wengine wa mahakama
Picha ya pamoja mgeni rasmi,majaji,mkuu wa wilaya ya Shinyanga,mawakili na wadau wa mahakama
Picha ya pamoja mgeni rasmi,majaji,mkuu wa wilaya ya Shinyanga,mawakili na waandishi wa habari
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog