WASANII WANAODAIWA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA WAANIKWA..YUMO WEMA SEPETU...MAJINA YA ASKARI 9 NAYO YAPO
Msanii
wa filamu nchini Wema Sepetu ametajwa kuwa ni kati ya wasanii ambao
wanatumia dawa za kulevya hivyo anapaswa kesho kukutana na Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda katika kituo cha polisi.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaama amewataja wasanii wengine akiwepo TID, Chid
Benz, pamoja na Recho na kusema anahitaji kesho wafike makao makuu ya
kituo cha polisi.
"Naomba
tukutane kesho pale polisi Central akiwepo TID, akiwemo Wema Sepetu,
wakiwepo wakina Junior Sniper, wakina Ditto, Titoo, kuna Ally Denya,
kuna wakina Chacha, kuna kina Mecky wengine hawa wakina Petit Man tayari
nishawatia mikononi mwa sheria, kuna watu kama kina Recho, Chid Benz
wote hawa nawahitaji ni vijana wenzangu nafikiri tutaelewana vizuri"
alisema Paul Makonda