Katika Kuadhimisha miaka 40 ya kuzaliwa chama cha Mapinduzi
(CCM) Wilayani Rorya Mkoani Mara Chama hicho kimesema kuwa hakitawafumbia Macho
viongozi wote kuanzia ngazi za Matawi, Mashina kata hadi Wilaya ambao wataendelea kukishika Miguu huku
wakienda Kinyume na Taratibu za uchaguzi
wa Jumuiya za CCM ambao unatarajiwa kufanyika Mwaka huu.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi
Wilayani Rorya Mkoani Mara Samwel Kiboye katika kongamano la kuadhimisha Miaka 40
ya kuzaliwa chama cha mapinduzi ambapo kongamano hilo limefanyika katika ukumbi
wa ofisi za chama hicho Wilaya.
|