TBS KUDHIBITI BIDHAA HAFIFU



Kaimu Mkurugenzi Mkuu  Shirika la Viwango Tanzania (TBS)  Prof. Egid Mubofu akizungumza na waandishi wa habari hawapo (pichani) kuhusu mafanikio ya Shirika hilo tangu Serikali ya awamu ya Tano iingie madarakani,Kushoto ni Afisa Uhusiano wa Shirika hilo Bi Roida Andusamile na kushoto ni Afisa Uhusiano Msaidizi Bi Neema Mtemvu.
. Kaimu Mkurugenzi Mkuu  Shirika la Viwango Tanzania (TBS)  Prof. Egid Mubofu akizungumza na waandishi wa habari hawapo (pichani) kuhusu mkakati wa shirika hilo kudhibiti uingizwaji na uzalishaji wa bidhaa hafifu hapa nchini.kushoto  Afisa Uhusiano wa Shirika hilo Bi Roida Andusamile.

Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia Mkutano wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) uliofanyika leo Jijini Dar es salaam ukilenga kueleza mikakati ya shirika hilo katika kutoa huduma bora kwa wananchi na kuchochea ujenzi wa uchumi wa Viwanda.


                         (Picha na Frank Mvungi).



Na: Lilian Lundo – Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  George Simbachawene amesema kuwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Simbachawene ameyasema hayo leo Bungeni, Mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la  nyongeza la Mbunge wa Jimbo la Chemba Juma Nkamia kuhusu Wakuu wa Wilaya na Mikoa kuwa wababe katika maeneo yao ya kazi.
“Wakuu wa Mikoa na Wilaya wanasimamia maeneo yao kwa mujibu wa sheria na wana haki ya kuwachukulia hatua watumishi ambao hawatekelezi majukumu waliyopewa,” alifafanua Simbachawene.
Aliendelea kwa kusema kuwa, hata kama kuna Wakuu wa Mikoa na Wilaya ambao ni wababe katika maeneo yao ya kazi hauwezi kusema kila Mkuu wa Mkoa au Wilaya aliyechukua hatua dhidi ya mtumishi ambaye hawajibiki katika kazi yake ni mbabe au muonevu.
Aidha, Simbachawene amesema kuwa ni wakati sasa wa watumishi wa Umma kutekeleza wajibu wao na kuacha kufanya kazi kwa mazoea. Kwani hakuna kiongozi ambaye ataweza kumchulia hatua mtumishi ambaye anawajibika na kazi zake kama alivyopangiwa.
Vile vile amesema kuwa, wakuu hao wa Mikoa na Wilaya wamekuwa wakifanya kazi nzuri katika maeneo wanayoyasimamia, kutokana na watumishi wengi wa Serikali walikuwa wamejisahau kutekeleza wajibu wao na kufanya kazi kimazoea.

Wabunge Wanawake Waadhimisha Miaka 40 ya CCM kwa Kufanya Mazoezi.



Na: Lilian Lundo - Dodoma.
Wabunge Wanawake, wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,    wameadhimisha miaka 40 ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kufanya Mazoezi ya Viungo vya Mwili katika Viwanja vya Jamhuri vilivyopo Mjini Dodoma.
Akiongea na Vyombo vya Habari alfajiri ya leo, mara baada ya kumaliza mazoezi hayo, Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson amesema kuwa wameamua kuadhimisha miaka 40 ya CCM kwa kufanya mazoezi kutokana na mazoezi humpa mtu furaha, upendo pia yanaunganisha watu.
Aliendelea kwa kusema kuwa, kufanya mazoezi kuna punguza  maambukizi ya magonjwa yasiyoambukiza hivyo ni vyema kila mmoja kufanya mazoezi kama ambavyo Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inavyosisitiza juu ya watanzania kufanya mazoezi ili kuepukana na magonjwa hayo.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura amesema kuwa imezoeleka katika jamii ya kitanzania kuona wanaume ndio washiriki wakubwa wa michezo na mazoezi lakini ukweli ni kwamba wanawake ndio wanaohitajika kufanya mazoezi zaidi kutokana na kuwa katika hatari kubwa ya kupata magonjwa yasiyoambukizwa kuliko wanaume.
" Ni wakati wa Watanzania kubadilika na kuwashilikisha watoto wa kiume kufanya kazi za nyumbani ili watoto wa kike nao wapate nafasi ya kushiriki michezo au mazoezi kama ilivyo kwa watoto wa kiume," alisema Anastazia Wambura.
Nae, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula amesema kuwa, mazoezi yamemsaidia awe na afya njema kutokana na kuwa mshiriki mzuri wa kufanya mazoezi kila siku.
Vile vile Mabula amesema kuwa, kufanya mazoezi kumemfanya aonekana kijana zaidi ya umri aliona, hivyo amewataka wanawake kumuunga mkono Makamu wa Rais Samia Suluhu kwa kupanua wigo wa kufanya mazoezi.

NHIF KUWAFIKIA ASILIMIA 85 YA WATANZANIA IFIKAPO 2020.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bw. Bernard Konga (kushoto)  akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam (hawapo pichani)  kuhusu maboresho yaliyofanywa na Mfuko. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Uhai wa Mfuko Bw. Baraka  Maduhu.

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw. Bernard Konga akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Bi. Angela Mziray na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Uhai wa Mfuko Bw. Baraka Maduhu.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bw. Bernard Konga (kushoto)  akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)  kuhusu ushiriki wa Mfuko katika kupunguza magonjwa yasiyoambukiza . Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Bi. Angela Mziray.
   Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bw. Bernard Konga (wa pili kutoka kushoto)  akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)  kuhusu ongezeko la usajili wa vituo vya kutolea huduma kwa wanachama wa Mfuko. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Uhai wa Mfuko Bw. Baraka Maduhu.


   Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia maelezo ya Kaimu Mkurugenzi wa NHIF Bw. Bernard Konga .
(Picha na Frank Mvungi)


Na Grace Michael

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umefanikiwa  kufikia makundi mbalimbali wakiwemo Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijijini Dar es salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bw. Bernard Konga amesema kuwa mafanikio haya yamefikiwa chini ya Serikali ya Awamu ya Tano ambayo imejipanga kuhakikisha zaidi ya asimilia 85 ya Watanzania wanakuwa kwenye Mfumo wa Bima ya Afya ifikapo mwaka 2020.

“Sisi kama Mfuko tunajivunia sana kufikia makundi mengi ya wananchi na kuyahudumia hususan kundi la waheshimiwa wabunge ambao awali hawakuwemo lakini pia kundi la watoto ambalo nalo ni muhimu sana,” alisema Bw. Konga.

Alisema kuwa kitendo cha Wabunge kuwa ndani ya huduma za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya utasaidia kwa kiasi kikubwa kwa kuwa wao ndio wawakilishi wa wananchi hivyo watasaidia kuwahamasisha wananchi kujiunga na Mfuko.

Bw. Konga alieleza kuwa pamoja na kuwepo kwa ongezeko la wanachama, Mfuko pia umeongeza usajili wa vituo vipya 92 na kufanya idadi ya vituo vinavyohudumia wanachama kuwa ni 6,998 hivyo kuwezesha kuwa na mtandao mpana wa huduma kwa wanachama wa NHIF.

Alitumia fursa hiyo pia kusema kuwa Mfuko umeshiriki kwa kiasi kikubwa kupunguza magonjwa hususan magonjwa yasiyoambukiza kutokana na kujikita katika utoaji wa elimu kwa wananchi ya namna ya kujikinga na magonjwa hayo lakini pia kuendesha zoezi la upimaji wa afyua bure katika maeneo mbalimbali vijijini.

“Tunao mpango wa elimu ya kata kwa kata ambapo kwa mwaka 2016 jumla ya kata 560 zilifikiwa na mpango huo hivyo sisi kama Mfuko tumetekeleza jukumu hili na tunaendelea kulifanya kupitia ofisi zetu za mikoani,” alisema.

Akizungumzia suala la uboreshaji wa miundombinu ya afya pamoja na ujenzi wa hospitali, Bw. Konga alisema kuwa, Mfuko umewekeza katika Vituo vya Kisasa vya uchunguzi wa magonjwa vilivyoko Dodoma na kutokana na uwekezaji huu umekwenda sambamba na mkakati wa Serikali wa Dodoma kuwa Makao Makuu ya nchi.

Alisema kuwa ujenzi wa Hospitali kubwa iliyopo Chuo Kikuu cha Dodoma inayojulikana kama Benjamin Mkapa imelenga kusaidia Serikali hasa katika kuondokana na gharama za kusafirisha wagonjwa nje ya nchi hivyo uwekezaji huo unayo manufaa makubwa kwa Watanzania kwa ujumla.

Aliwahakikishia wanachama wa Mfuko kuwa Mfuko uko imara na utawahudumia kwa kiwango kinachotakiwa kulingana na dhamana kubwa iliyopewa ya kutoa huduma za matibabu kwa wanachama wake.

“Mfuko uko imara kabisa, wanachama wajue hilo na sisi tunayo dhamana ya kulinda uhai wa Mfuko hivyo rai yetu ni kwa kila mwanachama ama Mtanzania kulinda huduma za Mfuko ili ziweze kutoka kwa walengwa na hatimaye kutimiza lengo lake.
Powered by Blogger.