KAIMU MKURUGEZI MTENDAJI WA TANESCO, DKT.TITO MWINUKA AKAGUA VITUO VYA KUPOZA UMEME VYA WILAYA YA TEMEKE NA KARIAKOO.
NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
KAIMU
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania, (TANESCO), Dkt.Tito
E. Mwinuka, (pichani kushoto), amefanya ziara ya kutembelea vituo vitatu vya kupoza na kusambaza
umeme wa msongo wa Kilovoti 132, (132Kv), vya Mbagala, Kurasini Wilayani Temeke
na Kariakoo Wilayani Ilala jijini Dar es Salaam leo Februari 4, 2016 na
kuwaomba wateja wa Shirika hilo kuwa wavumilivu wakati juhudi za kukamilisha
mradi wa uboreshaji umeme ukiwa unakaribia kukamilika.
Dkt.
Mwinuka alisema, ongezeko la watu na
shughuli za kiuchumi katika maeneo ya Mbagala, Kigamboni na Wilaya ya Mkuranga
Mkoani Pwani, kumepelekea upatikanaji wa umeme kwenye maeneo hayo kuwa na
matatizo kidogo kwani vituo vinavyosambaza umeme kwenye maeneo hayo vilikuwa na
ukubwa wa kupoza umeme wa Kilovoti 33 tu, na ndio maana TANESCO kupitia Mradi
wa uboreshaji umeme jijini Dar es Salaam unakaribia kukamilisha ujenzi wa vituo
vilivyotajwa hapo juu ili view na uwezo mkubwa wa Kilovoti 132 na hivyo kuondoa
kabisa tatizo hilo.
“Barabra
zinapozidiwa na magari ni rahisi sana kubaini kutokana na ongezeko la magari
yanayotumia barabara hizo, lakini ongezeko la watumiaji umeme na shughuli za
kiuchumi inakuwa vigumu kubaini kwa haraka, kwa hivyo niwaombe wateja wetu kuwa
wavumilivu kwani tatizo hilo litakuwa limepatiwa ufumbuzi katika kipindi kifupi
kijacho.” Alisema Dkt. Mwinuka.
Dkt.
Mwinuka pia aibainisha, kuwa kazi ya kuongeza ukubwa wa vituo vya kupoza na
kusambaza umeme inaendelea kwenye mikoa ya Mtwara na Lindi ambako nako vituo
vya sasa vya ukubwa wa Kilovoti 33, vinabadilishwa na kuwa na uwezo wa
Kilovolti 132.
Dkt.
Mwinuka amewapongeza wakandarasi kwa juhudi kubwa wanazofanya katika
kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa haraka ili kuwaondolea adha wateja wa
Shirika hilo wa upatikanaji wa umeme ulio bora na wa uhakika.
Dkt. Mwinuka (kulia), akipatiwa maelezo
ya litaalamu na Mkuu wa miradi (anayeshughulikia usafirishaji) wa
TANESCO, Mhandisi Frank Mashalo, alipotembelea kituo cha kupoza na
kusambaza umeme cha Mbagala, Wilayani Temeke jijini Dar es Salaam,
Februari 4, 2017. Wakwanza kushoto ni Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO,
Leila Muhaji.
Mitambo ya kupoza na kusafirisha umeme
kwenye kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kurasini jijini Dar es
Salaam, kikiwa katika hatua za mwisho ukamilika
Dkt. Mwinuka, (wapili kulia),
akimsikiliza mkandarasi kutoka kampuni ya FICHTNER, ambaye ndiyo Menenja
mradi, Mathias Alby, wakati alipotembelea kituo cha kupoza na kusambaza
umeme cha Mbagala, Wilayani Temeke jijini Dar es Salaam.
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Temeke,
Mhandisi Jahulula Maendeleo, (kushoto), akitoa maelezo ya kiutendaji kwa
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Dkt. Tito E.Mwinuka, wakati
wa ziara yake ya kutembelea vituo vya kupoza na kusambaza umeme vya
Mbagala na Kurasini vilivyoko Wilayani Temeka. Katikati ni Meneja
Mwandamizi wa TANESCO Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Mhandisi Mhandisi
Mahende Mgaya.
Dkt. Mwinuka (mbele), baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha Kurasini jijini Dar es Salaam.
Dkt. Mwinuka, (wapili kulia)
akimsikiliza Meneja Mwandamizi wa TANESCO anayeshughulikia miradi ya
usafirishaji na usambazaji umeme, Mhandisi Gregory Chegere, (kushoto),
wakati alipotembelea kituo cha Kurasini. Kulia ni
Meneja Mwandamizi wa TANESCO Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Mhandisi Mhandisi Mahende Mgaya.
Meneja Mwandamizi wa TANESCO Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Mhandisi Mhandisi Mahende Mgaya.
Muhandisi mwandamizi wa miradi wa
TANESCO, Mhandisi Rosmystice Luteganya, (kushoto), akizungumza na Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito E. Mwinuka, kwenye kituo cha
kupoza na kusambaza umeme cha Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Dkt. Mwinuka, (kulia), akikagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Fundi akiwa kazini kwenye kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kariakoo
Meneja Mwandamizi wa TANESCO Kanda ya
Dar es Salaam na Pwani, Mhandisi Mhandisi Mahende Mgaya, (aliyesimama),
akizungumza wakati wa majumuisho ya ziara hiyo, kwenye chuo cha TANESCO
jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Dkt. Mwinuka, Mhandisi Chegere na
Mhandisi Mashalo.
Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji (aliyesimama), akizungumza wakati wa kikao hicho.
Jengo la kituo cha bkupoza na kusambaza umeme wa msongo wa Kilovolti 132 cha Mbagala jijini Dar es Salaam, likiwa limekamilika
Meneja wa TANESCO Wilayani Temeke,
Mhandisi, Jahulula Maendeleo, (kulia), akizungumza na maafisa wa TANESCO
wakati wakimsibiri Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Dkt. Rito
E. Mwinuka kwenye kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Mbagala
jijini Dar es Salaam.