ASKARI POLISI 12 WATUMBULIWA KWA MADAWA YA KULEVYA TANZANIA
Kufuatia tuhuma zilizotolewa hivi
karibuni na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda
zikiwahusisha baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi kujihusisha na
biashara ya madawa ya kulevya, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP
Ernest Mangu amewasimamisha kazi Askari 12 waliotuhumiwa ili uchunguzi
ufanyike dhidi yao.
Akizungumza na vyombo vya habari muda mfupi uliopita, IGP Mangu alisema
ni lazima Jeshi la polisi lichukue hatua kali dhidi ya yeyote
atakayebainika kujihusisha na vitendo hivyo, hata kama ni askari.
"Jeshi la Polisi linachukua hatua madhubuti za kuwachunguza Askari na
Wasanii wote waliotuhumiwa na baada ya uchunguzi kumamilika hatua za
kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayethibitika kwa uhalifu
huo"alisema IGP Mangu.
Pia IGP Mangu ameiomba jamii kuendelea
kutoa taarifa za uhalifu wa aina yeyote ili nchi iendelee kuwa salama.
Hapo chini ni Majina ya Askari wanaotuhumiwa kujihusisha na biashara ya
Madawa ya kulevya, ambao wamesimamishwa kazi.