WAZIRI MKUU AONGOZA KUZINDUA DUKA LA BOHARI YA DAWA (MSD), MPANDA, MKOANI KATAVI.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (katikati),
akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka la Dawa la Bohari ya Dawa
(MSD), Mpanda mkoani Katavi. Kutoka shoto mwenye shati la kijani ni
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Katavi, Peter Mselemu,
Mkurugenzi wa MSD, Laurean Bwanakunu, Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Kanali
mstaafu Raphael Muhuga. Wa tatu kulia ni Waziri wa Nishati na Madini
Profesa Sospeter Muhongo.
Jiwe la Msingi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkurugenzi wa MSD, Laurean Bwanakunu wakifurahi wakiwa ndani ya duka hilo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkurugenzi
wa MSD, Laurean Bwanakunu na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo wakiwa meza kuu wakati wa uzinduzi wa duka hilo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa MSD.
Mwonekano wa duka hilo la MSD, mkoani Katavi.
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Kassim Majaliwa amesema utaratibu wa MSD wa kununua dawa moja
kwa moja kutoka kwa wazalishaji litaboresha upatikanaji wa dawa na
kupunguza gharama za kununua dawa kutoka nje ya nchi.
Amesema hayo wakati wa uzinduzi wa
duka la dawa la MSD, Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda, mkoani Katavi,
ambalo linaifanya MSD kuwa na jumla ya maduka 7 ya dawa nchini.
Waziri Mkuu pia amesema kwa mwaka huu
wa fedha shilingi Bilioni 251 zimetengwa kwa ajili ya ununuzi wa dawa
na vifaa tiba ili kupunguza changamoto za uhaba wa dawa na kueleza kuwa
shabaha ya serikali ni kufikia asilimia 95-100 ya upatikanaji wa dawa
hadi itakapofika mwezi Juni, 2017.
Kwa upande wake,Mkurugenzi Mkuu wa
MSD, Bwana Laurean Bwanakunu ameeleza kuwa duka hilo wataliendesha kwa
mwaka mmoja tu,na kisha kulikabidhi kwa Halmashauri ili iliendeshe na
kuongeza mapatao yao.
Kwa upande wa upatikanaji wa dawa,
Bwanakunu amesema kuwa kwa sasa fedha sio tatizo,na dawa zinaendelea
kuagizwa kulingana na mahitaji.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)