Timu ya Biashara United ya Musoma wachagua viongozi watakaoiongoza miaka 2
KLABU
ya michezo ya Biashara United, yenye maskani yake mjini Musoma,imefanya
uchaguzi wa kuwapata viongozi wapya watakaoingoza kwa kipindi cha miaka
2 huku uchaguzi huo ukifanyika kwa amani na utulivu wa hali ya juu. |
Viongozi wengine waliochaguliwa na nafasi zao kwenye mabano ni,Christiana Samo(Makamu Mwenyekiti),Elias Katogoro(Katibu Msaidizi),Ghat Marwa(Mweka Hazina),Marwa William)Meneja wa timu) huku wajumbe wa kamati ya utendaji waliochaguliwa ni,Shomari Binda,Augustine Mgendi,Melvin Nashon,Noar pamoja na Frenk Wabare.
Akizungumza mara baada ya kutangazwa kwa matokeo na Mwenyekiti wa uchaguzi huo,Said Gantala,Mwenyekiti mteule wa club hiyo,Selemani Mataso,aliwaomba viongozi wote waliochaguliwa kuhakikisha wanafanya kazi kwa kushirikiana ili kuweza kusukuma mbele maendeleo ya timu hiyo.
Alisema uongozi wa timu hiyo ni uongozi wa kujitoa hivyo ni vyema kila kiongozi aliyechaguliwa kuona jukumu la kuiongoza timu hiyo ni lake na asiachiwe mtu mmoja kufanya kila jambo kwani kufanya hivyom kutaifanya club hiyo kutokusonga mbele.
"Tumemaliza uchaguzi wa kuwapata viongozi kwa amani nakila mmoja amefurahi,sasa kilichobaki ni kufanya kazi kwa kushirikiana ili yale ambayo tumekusudia kuyafanya kwenye timu yetu yaweze kufanikiwa,"alisema Mataso.
Mjumbe wa Mkutano mkuu wa uchaguzi wa timu ya Biashara United,Frola Yongolo,akichangia jambo kwenye mkutano huo
Wajumbe wakifatilia mkutano
Mwenyekiti wa uchaguzi,Said Gantala,"Jecha"akionyesha kura iliyopigwa
Mijadala ikiendelea
Kura zikihesabiwa na wasimamizi wakiongozwa na "Jecha"
Uchaguzi ulikuwa si mchezo
Chini viongozi waliochaguliwa chini ya Mwenyekiti,Selemani Mataso