Mvua ambazo
zinaendelea kunyesha zikiambatana na upepo mkali katika Wilaya ya Rorya Mkoani Mara zinaendelea
kusababisha madhala makunbwa ambapo katika shule ya Sekondari Kisumwa Mvua
kubwa iliyonyesha Januari 28 mwaka huu imefanya uharibifu mkubwa uanaokadiliwa
zaidi ya Millioni 120 ambapo Mahabara Mbili zilianguka zote na chumba kimoja
kuezuliwa bati , Madarasa Mawili yameezuliwa bati na mbao zake huku madarasa
matatu yakiezuliwa upande mmoja hivyo
Majengo Nane yamekumbwa na janga hilo ukiwemo uharibifu wa vifaa vya mahabara
na na vifaa vya shule.
Joshua John ni Mwalimu Mkuu katika shule ya
Sekondari Kisumwa wilayani rorya Mkoani Mara amezidi kuiomba serikali kupitia
kamati ya maafa wilaya kulifanyia kazi suala hilo ili kumaliza
changamoto inayowakumba baada ya madarasa
kupungua na vifaa vya mahabara kuaribika .
Hata hivyo
amezidi kuwaomba Wadau wa maendeleo kujitolea ili kusaidia shule hiyo kwani
mali nyingi zimeaharibiwa vibaya.
|