TAASISI YA AGRI-BUSNESS MEDIA INITIATIVE YA JIJINI MWANZA YAWAHIMIZA VIJANA KUJIKITA KWENYE KILIMO.
Mkurugenzi wa
Taasisi ya Agri-Busness Media Initiative In Tanzania (AMI-TZ) ya Jijini
Mwanza, Deborah Mallaba, akikagua shamba la hekari mbili la taasisi hiyo
ambalo lina mkusanyiko wa matunda na mbogamboga za aina mbalimbali,
lililopo Igombe Ziwani, Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza.
Na Binagi Media Group
Taasisi ya AMI-TZ inajihusika na
kilimo cha matunda na mbogamboga kama vile matikiti maji, nyanya, bamia,
nyanya, pilipili mbuzi na aina nyinginezo nyingi.
Baada ya mavuno, taasisi hiyo hufanya
usindikaji wa mazao kwa ajili ya kuwafikishia wateja wake majumbani,
maofisini na mengine huuzwa moja kwa moja shambani.
"Baadhi ya vijana ukiwaeleza suala la
kilimo wanakuona kama vile umepitwa na wakati lakini wale wanaojitambua
wameingia kwenye kilimo na kinawalipa. Hivyo niwahamasishe watumie muda
wao vizuri kwa kujishughulisha kwenye kilimo hivyo wasisubiri tu kazi
za maofisini". Anasisitiza Deborah Mallaba, Mwanahabari na Mkurugenzi wa
Taasisi ya AMI-TZ.
Mallaba anawasisitiza viongozi wa
serikali kuanzia ngazi ya Kata hadi Wilaya, kuongeza jitihasa za
kuwakusanya vijana pamoja na kuwapatia mitaji ikiwemo pembejeo ili
wajikite kwenye kilimo maana kilimo ni biashara na kinalipa ambapo pia
hatua hio itasaidia kupunguza vijana mitaani.
"Napenda kuwaambia akina dada waamuke
maana si vyema kuzurura tu wakisema hakuna ajira. Mfano mimi nimeanza
kujiwekea kipato changu kupitia kilimo na nataka kuwa mafano bora kwa
vijana wengine". Anasisitiza Aneth
Shosha ambaye ni Afisa Masoko wa taasisi ya AMI-TZ huku akiwakaribisha
vijana wengine kwenye taasisi hiyo ili wajifunze zaidi kuhusu kilimo.
Umwagiliaji kwenye shamba la bamia, kilimo hiki kinategemea maji kutoka ziwa victoria hivyo kinafanyika msimu wowote kwa mwaka.
Aneth Shosha
ambaye ni Mratibu/ Afisa Masoko wa Taasisi ya Agri-Busness Media
Initiative In Tanzania (AMI-TZ), akimwagilia maji kwenye shamba la bamia
Ukaguzi wa mbogamboga kila siku ni
kanuni ambayo husaidia kutambua mmea unaoanza kushambuliwa na wadudu ili
kwahi umwagiliaji wa dawa hususani dawa asilia
Wachapa kazi wakichakarika
Umwagiliaji wa kwenye kilimo cha nyanya
Kilimo cha matikiti maji
Kilimo cha nyanya
Kilimo cha bambia
Mfumo wa umwagiliaji kwa kutumia mashine kutoka Ziwa Victoria ndio hutumika kwenye shamba hili.