Kata ya Nkome wilaya na Mkoa wa Geita,kumefanyika
uchaguzi mdogo wa udiwani huku hali ya ulinzi na usalama ikitawala katika
kipindi chote cha upigaji wa kura.
Madukaonline imezungumza na msimamizi mkuu wa uchaguzi
ambaye ndie Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Geita,Ali Kidwaka ambapo
ameelezea kuwa zoezi hilo limefanyika katika hali ya utulivu na kwamba jumla ya
vituo therasini na nane (38)vimeusika kufanya uchaguzi.
“Zoezi la kupiga kura limeanza saa moja kamili ndio
vituo vimefunguliwa na nimefanikiwa kuzungukia vituo vyote Therasini na
nane kwasababu uchaguzi unafanyika hapa
Nkome katika vituo Therasini na nane na katika vituo nilivyozungukia hakukua na
matatizo ya vivaa na wananchi
wameendelea kupiga kura kwa uhuru Kabisa”Alisema Kidwaka.
Kuhusu swala la ulinzi na usalama Kidwaka amesema kuwa
hali ilikuwa tulivu hakuna fujo au usumbufu wowote ambao umeweza kujitokeza
lakini nje ya vituo kuna maswala yalijitokeza ya uvunjifu wa amani na utulivu.
Madukaonline imezungumza na Baadhi ya wananchi wa kata
hiyo,Hussein Omary ameeleza kuwa uchaguzi ambao umefanyika uko katika hali
nzuri kwani hayupo ambaye ameshindwa kupiga kura vituo vyote vilikuwa wazi na
kwamba kila mtu alikuwa ana uhuru wa kumchagua Yule ambaye anaona yupo sahihi
kumwongoza.
Bi,Flora Mussa amesema kuwa wao kama wazee
wanaishukuru serikali kwani hakuna buguza ambayo wamekutana nayo na kwamba
wamekuwa wakipewa nafasi ya upendeleo na kuthaminiwa katika chumba cha
uchaguzi.
Kwa mujibu wa msimamizi mkuu upigaji kura unatarajia
kumalizika saa kumi kamili(10:00)na matokeo yatatangazwa Majira ya saa Moja
kamili jioni(1:00)
IMEANDALIWA NA MADUKAONLINE