NAIBU WAZIRI WA AFYA ASHIRIKI MAULIDI YA KUZALIWA MTUME MUHAMMAD JIJINI DAR.



Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na wageni mbalimbali wakati akiwasili kwenye hafla hiyo ya maulidi ya Mtume.
Na Andrew Chale

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na wageni mbalimbali katika tukio hilo

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla akijadiliana jambo na wageni waalikwa wengine katika tukio hilo akiwemo Prof. Ibrahim Lipumba

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na wageni katika hafla hiyo ya maulidi ya Mtume

Baadhi ya vijana wa Madrasa mbalimbali kutoka Dar es Salaam na baadhi ya mikoa wakifuatiliatukio hilo

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Naibu waziri wa Tamisemi, Mh. Suleiman Jafo wakati akiwasili kwenye hafla hiyo ya maulidi ya Mtume

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla akijadiliana jambo na Naibu waziri wa Tamisemi wakati wakiwasubiria wageni waalikwa akiwemo Rais Mstaafu wa awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi pamoja na Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal wakati wa kumpokea alipowasili kwenye hafla hiyo.

Dua zikiendelea

Dua zikiendelea

Rais Mstaafu wa awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi ambaye alikuwa mgeni rasmi, akizungumza katika tukio hilo
Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akipokea zawadi kwenye hafla hiyo.
Dk. Kigwangalla akipokea zawadi katika hafla hiyo
Wageni mbalimbali wakifuatilia hafla hiyo ya Maulidi

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla leo 22 Januari 2017, ameshiriki Maulid ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW), iliyoandaliwa na kampuni ya Nida Textile Mills Ltd.
Pia hafla hiyo mgeni rasmi alikuwa Rais Mstaafu wa awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi pamoja na viongozi wengine mbalimbali wa kiserikali akiwemo Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na viongozi wa Dini nchini. 
Katika hafla hiyo, Al-Haji Ali Hassan Mwinyi amewataka watanzania kuwa na tabia ya kuyafanyia muendelezo yale mema wanayoyafanya, kama walivyofanya kampuni hiyo ya Nida na kuwakutanisha pamoja waislamu na kumsifu katika kumbukumbu hizo za kiongozi wa waislamu Mtume Muhammad (S.A.W).
Mbali na Dk. Kigwangalla, wageni wengine ni pamoja na Naibu Waziri Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleiman Jafo, Waziri wa zamani wa Ulinzi Profesa Juma Kapuya, Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahimu Lipumba, Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega huku kwa viongozi wa dini walikuwepo Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum na Kadhi Mkuu wa Tanzania Abdallah Mnyaa ambapo wote kwa pamoja walipewa zawadi maalum na kampuni hiyo.
Powered by Blogger.