Polisi Mara yapata ushindi wa 1-0 dhidi ya Polisi Dodoma





POLISI Mara imetamba nyumbani kwanza kwa kupata ushindi wa bao 1-0 kuitandika Polisi Dodoma katika mchezo uliofanyika jana jumamosi katika uwanja wa Karume mjini Musoma.

Bao  pekee la Polisi Mara lilipatikana  kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 37 kupitia kwa mshambuliaji Kaisi Pastory aliyefunga bao hilo na kuwainua mashabiki kwenye viti vyao.

Bao hilo lilidumu kwa muda wote wa mcheo huo hadi dakika 90 zilipomalizika matokeo hayakuweza kubadilika na kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Kocha mkuu wa Polisi Mara, Henry Mkanwa akiwa amejawa furaha alisema ndio mwanzo wa kufanya vizuri baada ya kufanya vibaya kwenye mechi zilizopita na zinazofuata  makosa yaliyopo atayarekebisha.

“Matokeo haya ni baada ya kufanyia kazi makosa yaliyokuwepo kwnye kikosi, maana wakati nakipokea kilikuwa kibaya sana hasa kwenye umaliziaji, kwa mechi zilizotangulia nilikuwa nikisoma kikosi na kuona mapungufu,” alisema Mkanwa.

Alisema kuwa siri ya ushindi wao ni uongozi kuanza kusikiliza matakwa ya timu na kuyatekeleza mahitaji yake kwa wakati ambapo pia wacheaji wa kikosi hicho wamepata mwamko wa kujituma.

“Bado hawakufanya vizuri kama nilivyotaka tulitakiwa kupata mabao mengi makosa ya umaliziaji nimeyaona na nitayafanyia kazi ili kuimaisha kikosi zaidi,” alisema Mkanwa.

Alisema kuwa timu ya Polisi Dodoma anaifahamu vizuri kwani alikuwa Kocha wake, ndiyo maana alitumia udhaifu wao kupata ushindi.

“Mashabiki wetu wajue kuwa huu ni mwanzo wa kuwapa furaha timu iko vizuri na imenza mwendo kulekea kufanya vizurri kwenye mechi zinazofuata,” alisema Mkanwa.


Powered by Blogger.