Tarime United noma, yaichapa Tarime Warriors 2-1




TARIME United imeichapa Tarime Warriors mabao 2-1 kwenye mchezo wa kupimana nguvu uliopigwa mwishoni mwa wiki (jumamosi) katika uwanja wa Serengeti mjini hapa.

Tarime Warriors ndio walitangulia kupata bao la kuongoza katika dakika ya 25 kupitia kwa Hamis Moshi na kuegeuza upepo wa mchezo huo  kuifanya Tarime United kushambulia kwa nguvu zote.

Mashabulizi hayo yalizaa matunda dakika ya 39 kwa Godson Daudi kuipatia timu yake bao la kusawaisha na kuongeza bao la pili na la ushindi katika dakika ya 82, dakika nane kabla ya mchezo huo kumalizika.

Kocha wa Tarime Warriors William Oremo alisema timu yake iko vizuri na vijana wako katika hali nzuri na matokeo hayo ndiyo hali halisi ya mchezo nimeyapokea na kwenda kufanyia marekebisho mapunufu niliyoyaona.

“Wenzetu wamepata nafasi wameitumia vizuri na kufunga bao la usindi, lakini kikosi changu kiko imara na kinafanya vizuri ukizingatia kuwa vijana wetu wako chini ya umri wa miaka 20 (U20),” alisema Oremo.

Kwa upande wake, kocha wa Tarime United Hamis Bakari alitanda kutokana na ushindi huo kuwa kikosi chake kinauwezo mkubwa ndio maana kilipatta ushindi.

“Timu yangu umeiona iko vizuri ndio maana tumetanguliwa kufungwa lakini tumesawazisha na kuongeza bao la ushindi,” alisema Bakari.
Mwiso.



Powered by Blogger.