Waumini wa dini ya Kiislamu wametakiwa Kuendelea kuswali
ikiwa ni pamoja na kufanya kazi za uzalishaji ili kujiletea maemndeleo kama
maandikomatakatifu yanavyosema ikiwa ni pamoja na kuwa na mashikamano wa pamoja
kwa lengo la kuwasaiadia watu wenye mahitaji, Wakiwemo Walemavu, Wajane pamoja
na Yatima.
Akifungua Rasmi Mashine Tatu za Kusaga katika Msikiti Mkuu
wa Ijumaa Wilayani Tarime Mkoani Mara Sheikh Mkuu kutoka Mkoa wa Shinyanga
Ismail Habibu Makusanya alisema kuwa Waumini wa Kiislamu wanawajibu mkubwa wa kendelea kuswali ikiwa ni pamoja na
kufanya kazi za uzailishaji kama maandiko matakatifu yanavyosema.
Hata hivyo Sheikh huyo aliongeza kuwa dini ya kiislamu bado
inaimia kufanya kazi pamoja na kufanya baishara kwa lengo la kujipatia
riziki hivy amezidi kuwasisitiza waumini
wote kuendelea kufanya kazi kwa ajili ya kuijipatia kipato
Hizi mashine Tatu zaidi ya Millioni 20 siyo haba ni kazi
kubwa mliyofanya na watu wengine wanapaswa kuiga mfano wa waumini wa kiislamu
wilaya ya Tarime kwani ni waumini pekee waislamu wa ujasiriamli pamoja na
uzalishaji.
Awali wakisoma Risla mbele ya Sheikh huyo walisema kuwa
awalia kamati ya IQRA EDUCATION FUND
mnamo mwaka 2009 iliwezakununu kiwanja na ilipofika mwaka 2013 ikileta wazo la
kujenga na kuweka mradi wa mashine tatu kutokana na nguvu za waislamu wa Tarime
kwa asilimia99% ambapo ghalamaza ununuzi wa kiwanja zilikuwa 7,000,000 pamoja na
usajili wa kiwanja hicho, ujenzi kutoka msingi hadi jingo kukamilika
limegahalimu 10,294,086 pamoja na Mradi wa amshine Mbili za kusaga na moja ya
kukoboa zimeghalimu shilingi 9,291,986
hivyo kufanya ghalama zote toka mwanzo
hadi sasa kufikia shilingi 26,576,072.
|