MLIMBWENDE WA SHINDANO LA MISS KIBOSHO 2017 JIJINI MWANZA APATIKANA.
Baada ya mtifuano mkali wa kumtafuta
mlimbwende wa shindano la MISS KIBOSHO 2017 kufanyika kwa mara ya kwanza
usiku wa ijumaa Januari 27,2017 na jana jumamosi Januari 28,2017 katika
Ukumbi wa Kibosho Luxury Bar Kiseke Ilemela Jijini Mwanza, hatimaye
mshindi amejulikana.
Mshindi wa shindano hilo lililofana
vyema alikuwa ni Kephlin Jacob (katikati), nafasi ya pili ni Aida Gazar
(kulia) na nafasi ya tatu ni Caren Nestory (kushoto), ambapo wanyange
hao walifanikiwa kupenya na kuibuka na ushini huo miongoni mwa wanyange
10 walioshiriki shinano hilo.
Miss Kibosho 2017 iliandaliwa na Raju
Entertainment kwa ushirikiano wa karibu na Kibosho Luxury Bar and Guest
House Kiseke, Wema Salon, Mama Ngenda Sakon, Top Model na Hangano
Cultural Group lengo lake ikiwa ni kukuza vipaji vya urembo kitaifa na
kimataifa.
Na Binagi Media Group
Miss Kibosho 2017 Kephlin Jacob
(katikati), Miss Kibosho 2017 nambari mbili, Aida Gazar (kulia) na Miss
Kibosho nambari tatu ni Caren Nestory (kushoto).
Miss Kibosho 2017 Kephlin Jacob
(katikati), Miss Kibosho 2017 nambari mbili, Aida Gazar (kulia) na Miss
Kibosho nambari tatu ni Caren Nestory (kushoto).
Matron wa Miss Kibosho 2017, Fania Hassan ambaye pia ni Miss Utalii 2006 (katikati), akimvisha taji Miss Kibosho 2017
Awali hatua ya tatu bora ilikwena kwa washiriki, Caren Nestory (kushoto), Kephlin Jacob (katikati) na Aida Gazar (kulia)
Awali washiriki waliotinga nafasi tabo bora ni Caren Nestory, Jackline Moses, Denzry Michael, Kelphine Jacob na Aida Gazar.
Washiriki wote 10 wa Miss Kibosho 2017
ambao ni Caren Nestory, Dorice Ezra, Jullieth Michael, Elizabeth
Faustine, Christina Lucas, Nasra Ramadhan, Jacline Moses, Denzry
Michael, Kephlin Jacob na Aida Gazar.
Matroni wa Miss Kibosho 2017, Fania Hassan ambaye pia ni Miss Utalii 2006, akiwa na washiriki wa shindano hilo
Awali Jaji Mama Ngenda Lutalo (katikati)
akiwauliza maswali washiriki wa Miss Kibosho 2017. Majaji wengine ni
Leonald Kaduguda (kushoto) na Mwalimu wa ulimbwende, Tatu Ngelangela
(kulia)
Washiriki wa Miss Kibosho 2017 wakiwa
katika picha ya pamoja na waandaaji wa shindano hilo, uongozi wa Kibosho
Luxury Bar & Guest House
Washiriki wa Miss Kibosho 2017 wakiwa
katika picha ya pamoja na waandaaji wa shindano hilo, uongozi wa Kibosho
Luxury Bar & Guest House pamoja na mpambaji Wema Salon (wa kwanza
kushoto).
Mwanamuziki na mcheza ngoma za asili kutoka Hangano Cultural Group akitumbuiza
Majaji wakitoka kumtuza mwanamuziki na mcheza ngoma za asili kutoka Hangano Cultural Group
Kushoto ni Jaji wa Miss Kibosho 2017 na
kulia ni Mkurugenzi wa Kibosho Luxury Bar & Guest House, wakicheza
pamoja na mwanamuziki na mcheza ngoma za asili kutoka Hangano Cultural
Group (katikati).
Kulikuwa na muziki mnene balaa