CHUO CHA AFRICA GRADUATE UNIVERSITY CHAWATUNUKU PhD WANAOFANYA KAZI ZA JAMII NCHINI.
Mkuu wa Chuo cha Africa Graduate
University cha jijini Dar es Salaam, Profesa Stiven Nzowa, akiongoza
mahafali ya kuwatunuku Tuzo ya Heshima ya Udaktari (PhD) wanaharakati na
watumishi wa mungu nane pamoja na wengine kadhaa waliotunukiwa Tuzo ya
Heshima ya Shahada ya Uzamili HDD Dar es Salaam jui.
Mwanaharakati wa
Haki za Watoto ambaye ni Rais wa Tanzania Music Foundation Dk.Donald
Kisanga aliyetunukiwa PhD ya masuala ya Usimamizi na Uongozi wa Biashara
akiwa kwenye mahafali ya 30 ya Chuo cha Africa Graduate University
yaliyofanyika Dar es Salaam juzi
Askofu Dk. Godfrey
Mallasy wa Kanisa la Tanzania Fellowship of Churches, akielezea kazi
mbalimbali alizofanya kabla ya kutunukiwa tuzo hiyo.
Waliotunukiwa tuzo wakiwa na furaha katika picha ya pamoja.
Wageni waalikwa wakiwa na Mama Askofu
Dk.Godfrey Mallasy, Debora Mallasy (mwenye kofia), alikuwepo kushuhudia
mume wake akitunukiwa tuzo hiyo.
Meneja Programu na mshereheshaji katika mahafali hayo,
Lucy Wilson akiwa kazini.
Watunukiwa tuzo hao wakiingia ukumbuni.
Wimbo wa Taifa ukiimbwa.Katikati ni
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Salum Hamdun ambaye alikuwa
mgeni rasmi kwenye mahafali hayo. Kushoto ni Mkuu wa chuo hicho,
Profesa Stiven Nzowa na kulia ni mke wa Makamu Mkuu wa Chuo cha Africa Graduate University, Profesa Timothy Kazembe.
Mama Askofu Dk.Godfrey Mallasy, Debora Mallasy akiomba kabla ya kuanza kwa mahafali hayo.
Mkaguzi wa Polisi (ASP) Ezekiel Kyogo akionesha moja ya kitabu alichokiandika chenye manufaa kwa jamii. Kyogo alitunukiwa PhD.
Meneja Takwimu Mkoa wa Arusha Margaret Mutaleba, akieleza kazi alizozifanya katika jamii.
Wageni waalikwa wakiwa kwenye hafla hiyo.
Wasanii wa Bendi ya Jordan wakitumbuiza katika mahafali hayo.
Mwanahabari Tumaini Msowoya, akieleza kazi alizoziandika ambapo zimekifanya chuo hicho kumtunuku Tuzo hiyo ya Heshima.
Watoa huduma katika mahafali hayo, wakiwa katika picha ya [pamoja na Meneja Programu, Lucy Wilson.
Makamu Mkuu wa Chuo cha Africa Graduate
University, Profesa Timothy Kazembe (kulia), akimtunuku Tuzo ya Heshima
ya Udaktari (PhD), Askofu Dk. Godfrey Mallasy katika mahafali hayo.
Makamu Mkuu wa Chuo
cha Africa Graduate University, Profesa Timothy Kazembe (kulia),
akimtunuku Tuzo ya Heshima ya Udaktari (PhD), Meneja Takwimu Mkoa wa Arusha, Margaret Mutaleba.
Makamu
Mkuu wa Chuo cha Africa Graduate University, Profesa Timothy Kazembe
(kulia), akimtunuku Tuzo ya Heshima ya Udaktari (PhD), Godwin Maimu.
Makamu Mkuu wa Chuo
cha Africa Graduate University, Profesa Timothy Kazembe (kulia),
akimtunuku Tuzo ya Heshima ya Udaktari (PhD), Donald Kisanga.
Makamu
Mkuu wa Chuo cha Africa Graduate University, Profesa Timothy Kazembe
(kulia), akimtunuku Tuzo ya Heshima ya Udaktari (PhD), Mwanahabari
Tumaini Msowoya.
Furaha na tabasamu baada ya kutunukiwa tuzo hiyo.
Watunukiwa tuzo hizo, Dk.Donald Kisanga
(kushoto) na Mkaguzi wa Polisi (ASP), Ezekiel Kyogo (kulia), wakiwa na
jamaa zao baada ya kutunukiwa tuzo hiyo.
Viongozi wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania, Dk.Godwin Maimu (kushoto) na Dk.Donald Kisanga wakiwa katika picha ya pamoja.
Na Dotto Mwaibale
CHUO cha Africa Graduate University
cha jijini Dar es Salaam kimewatunuku Tuzo ya Heshima ya Udaktari (PhD)
wanaharakati na watumishi wa mungu nane pamoja na wengine kadhaa
waliotunukiwa Tuzo ya Heshima ya Shahada ya Uzamili HDD.
Watumishi waliotunukiwa tuzo hizo za
heshima ni wale waliotoa mchango mkubwa kwa kufanya shughuli mbalimbali
za kujitolea za kijamii na zikaleta manufaa kwa mtu mmoja mmoja na taifa
kwa ujumla.
Akizungumza katika mahafali ya 30 ya
chuo hicho chenye makao makuu yake Sierra Leone, Mkuu wa Chuo hicho,
Profesa Stiven Nzowa alisema kila mwaka chuo hicho kimekuwa kikitoa Tuzo
za heshima na Shahada za Uzamili kwa watanzania waliotoa mchango wa
kusaidia jamii katika shughuli mbalimbali.
"Tunao watunuku tuzo hizi tuzo za
heshima ni watu waliokuwa na umri wa miaka 60 ambao wanafanya kazi za
kijamii katika nyumba za ibada kwa zaidi ya miaka 15 na kuendelea na
wale ambao umri wao ni miaka 40 hadi zaidi na wenye shahada" alisema
Profesa Nzowa.
Wakizungumzia kazi walizozifanya
katika jamii Askofu Dk. Godfrey Mallasy wa Kanisa la Tanzania Fellowship
of Churches alisema amefanyakazi nyingi za kijamii ikiwemo kusaidia
watoto wanaoishi katika mazingira magumu na yatima na kubwa zaidi kwa
kipindi cha miaka 20 amekuwa akifanya mkesha mkubwa wa kuliombea taifa
amani na yeye akiwa ni mhasisi.
"Kazi hii ya kuliombea taifa amani
tulianza mwaka 1997 na tumeweza kupeleka huduma hiyo hadi Zanzibar
ambako kumefanyika maombi hayo kwa miaka saba na kuifanya Tanzania kuwa
na amani" alisema Dk. Mallasy.
Mwanaharakati wa Haki za Watoto
ambaye ni Rais wa Tanzania Music Foundation Dk.Donald Kisanga
aliyetunukiwa PhD ya masuala ya Usimamizi na Uongozi wa Biashara alisema
amefanya kazi nyingi za kijamii ikiwa pamoja na kuishawishi serikali
kukagua fedha zinazotolewa na wahisani kwenye taasisi mbalimbali
zinazojishughulisha na kuwatunza watoto yatima baada ya kubaini baadhi
yake zimekuwa zikifuja fedha bila ya kuwasaidia walengwa.
Mwingine aliyetunukiwa tuzo hiyo ya
heshima ni Meneja Takwimu Mkoa wa Arusha Margaret Mutaleba ambaye pamoja
na kufanya shughuli nyingi za kijamii pia ndiye aliyemshauri Rais Dk.
John Magufuli kuhusu mpango wa kufanya usafi ambao unaendelea
kutekelezwa nchini kote.
Mbali na watu hao kutunukiwa tuzo
hiyo ya heshima yupo mwanahabari mahiri wa gazeti la Mwananchi, Tumaini
Msowoya ambaye ametunukiwa PhD kutokana na kufanya kazi mbalimbali za
kijamii kupitia kalamu yake ambazo zimeleta mrejesho mkubwa kwa walengwa
na kuweza kusaidiwa.
Waliotunukiwa tuzo ya heshima ya udaktari ni Donald Kisanga, Mlute Nyasa, John Pallangyo, Wilson Nyiti na Godwin Maimu.
Wengine ni Askofu Dk. Godfrey
Mallasy, Ofisa wa Jeshi la Polisi Ezekiel Kyogo, Mtakwimu Margaret
Mutaleba na Mwanahabari Tumaini Msowoya.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)