|
Timu ya Bukoli FC wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo kuanza |
|
Timu ya Bomani kutoka mjini Geita wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo kuanza. |
|
Kaimu
Mgeni Rasmi ambaye ni Diwani wa Bukoli Faraji Seif akikagua vikosi na
kusalimiana na wachezaji wa timu zote mbili yaani Bukoli Fc na Bomani |
|
Mgeni Rasmi akiongozwa na kapteni wa timu ya Bukoli Fc akisalimiana na wachezaji wa timu hiyo kabla ya mchezo kuanza. |
|
Mh,Faraji
Seif ambaye ndiye mgeni rasimi kwenye uzinduzi wa ligi daraja la nne
wilaya ya Geita akifatilia kwa makini mchezo uliokuwa ukiendelea
uwanjani |
|
Mlinda mlango wa timu ya Bomani akitoka nje baada ya kuwa amepata majeraha katika mchezo huo. |
|
Mlinda mlango akiwa amebebwa . |
|
Baadhi ya mashabiki wakiendelea kufatilia kwa umakini mechi ambayo ilikuwa inaendelea uwanjani. |
|
Mashambulizi yakiendelea kwa kasi kubwa kwenye viwanja vya bukoli |
|
Mwamuzi wa mchezo huo , Majeshi Mgema akitoa maelekezo kwa wachezaji wa timu ya Bomani. |
MADUKAONLINE
Mashindano ya
Soka Ligi daraja la nne (4) ngazi ya wilaya ya Geita yameanza kutimua
Vumbi jana ambapo Mechi ya Ufunguzi ilikuwa kati ya Bukoli FC dhidi ya
Bomani FC na Mshindi ameibuka Bukoli kwa goli tatu(3)didi ya Bomani
kutoka mjini Geita.
Ilikiuwa siku
ya jana January 19,2017 majira ya jioni ambao Historia imeandikwa kwa
mala ya kwanza baada ya miaka ishiriki ( 20)kupatikana kwa kituo cha
ufunguzi wa Ligi daraja la nne ngazi ya wilaya.
Akifungua
mashindano hayo kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Geita Mwl,Herman Kapufi
ambaye alitarajia kuwa mgeni rasmi Diwani wa Kata ya Bukoli Faraji
Seif,aliwataka wachezaji kuwa na nidhamu ya hali ya juu katika kipindi
chote cha ligi huku akiwataka mashabiki kuwa na nidhamu katika swala la
ushangiliaji.
“Natambua kuwa
michezo ni ajira ni vyema kutumia nafasi hii kwa kujituma kwa timu zote
ambazo zitashiriki ligi hii na niwaombe sana wale ambao mtashindwa
mkubali kushindwa maana mchezo ni dakika sitini(90) kwa hiyo hatutarajii
kuona mnakuwa sio watu wa kuheshimiana jambo la msingi wasikilizeni
walimu wenu nikiwa na maana makocha na pia muwe watu wa kujituma kwenye
mazoezi naamini mkizingatia haya basi mtafanya vizuri timu
zote”aliwasisitiza Seif
Katika mechi ya
ufunguzi wenyeji Bukoli waliitandika Boman FC mikwaju mitatu dhidi
ya miwili katika kipindi cha pili .katika mchezo huo uliochezeshwa na
mwamuzi Majeshi Mgema.
Mabadiliko
makubwa yalionekana katika kipindi cha pili ambapo timu zote zilionesha
ushindani na kucheza kwa kukamiana ambapo kunako dakika ya hamsini(50)
mchezaji Shukuru Mtesiga aliiandikia bao la kwanza Bukoli FC, na dakika
ya hamsini na saba (57) mchezaji mwenzake Marius Joseph akafunga goli
la pili
Bomani FC
wakapata goli la kwanza katika dakika ya sitini na saba ( 67 )kupitia
kwa mchezaji wao Kasaba Sabu,na dakika ya sabini na saba (77)kwa mara
nyingine Shukuru Mutesiga aliyeonekana kinara katika mchezo huo
akaipatia ushindi timu ya Bukoli kwakuzamisha mpira kimiani na kuandika
bao la tatu(3). Goli la pili la Bomani lilipatikana kunako dakika ya
themanini na mbili (82 )kupitia kwa mchezaji John